Man United mbioni kufunga kamera kwenye jezi za wachezaji

Man United mbioni kufunga kamera kwenye jezi za wachezaji

‘Klabu’ ya Manchester United imepanga kuwawekea wachezaji wao ‘kamera’ katika ‘jezi’ wakati wa ‘mechi’ kwa lengo la kuruhusu mashabiki kutazama kwa karibu uwezo wa wachezaji wanaowapenda.

Uamuzi huu umefanywa na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani Ed Woodward, na familia ya Glazer ili mashabiki waweze kutoa mtazamo wao kwa mchezaji mmoja mmoja na kuwapa furaha mashabiki hao.

Hata hivyo, utekelezaji wa teknolojia hii unakabiliwa na changamoto za udhibiti, kwani sheria za sasa za #IFAB zinazuia wachezaji kuvaa vifaa hivyo wakati wa ‘mechi’ za mashindano, ingawa ‘Ligi’ Kuu Uingereza iko wazi kwa kuchunguza njia za kuwaleta mashabiki karibu na wachezaji wanaowakubali.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags