Mambo yakuzingatia unapoalikwa kwenye sherehe

Mambo yakuzingatia unapoalikwa kwenye sherehe

Glorian sulle

Uchaguzi wa vazi la kwendea harusini kama mwalikwa unahitaji uangalifu mkubwa sana, ni muhimu kuvaa vazi ambalo litakufanya ujisikie vizuri mwenye kujiamini na hasa liwe ndani ya maudhui ya sherehe husika.

Vazi la heshimu kama suti kwa wanaume au gauni zuri kwa wanawake mara nyingi ni chaguo bora kulingana na maudhui ya sherehe.

Unachohitaji kufahamu ni kuwa kama mwalikwa unatakiwa kuwa na vazi la heshima na litakalokupa kujiamini kwako na kwa wengine.

Kila sherehe ina maudhui yake ya kimavazi kulingana na inapofanyikia, mfano sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa na inapofanyikia ni ufukweni, kila mmoja anajua ni yepi mavazi stahiki katika shehere hiyo.

Ndivyo pia kwenye  aina nyingine za sherehe inapaswa tufahamu ni yapi mavazi sahihi  yanayotunza maudhui ya sherehe husika na kukupa kujiamini.

Awali sherehe za harusi na nyinginezo , waalikwa walikuwa wanavaa mavazi marefu yenye stara, walijua kutofautisha maudhui ya sherehe hivyo hakukuwa na sintofahamu kuhusu mavazi pindi wanapokuwa ukumbini.

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mkaanganyiko wa mavazi kwa waalikwa hasa kwa kushindwa kutofautisha nini avae kulingana na maudhui ya sherehe husika.

Ili utegue kitandawili hiki cha nini uvae unapoalikwa katika sherehe, kuna mambo muhimu ya kuzingatia  ambayo yatakupa kujiamini katika sherehe hiyo.

Maudhui na utaratibu wa sherehe,

Unapoalikwa kwenye sherehe cha kwanza angalia maudhui ya sherehe na utaratibu wake kama ni sherehe rasmi au isiyo rasmi mavazi yanapaswa kufuata miongozo ya mwenyeji au mwalikaji na aina  gani ya sherehe.

Kikawaida tunafahamu harusi inakuwa na waalikwa wa aina mbalimbali wakubwa kwa wadogo na viongozi wa dini, kwa kuzingatia hilo itakupasa uvae mavazi ya stara uendapo ukumbini hii itakupa uhuru na kujiamini wakati wote.

Mazingira ya ukumbi

Elewa mazingira ya ukumbi au eneo la sherehe, kama ni ndani au nje, hii itakusaidia kufanya chaguo sahihi la nguo kama mwalikwa

Huwezi vaa suti na kwenda kufanya sherehe kwenye mabwawa yakuogelea lakini pia ukavaa mavazi ya kuogelea ukumbini au mavazi ya kwenye kumbi za starehe ukaenda nayo kwenye harusi, pengine ukavaa pensi kwenye harusi unapaswa kufanya chaguo sahii kwa kuzingatia hayo.

Heshima na adabu, katika chaguzi zako za mavazi hakikisha unachagua vazi la heshima litakalokuheshimisha wewe,  wenyeji na wageni pia, epuka mavazi yasiyo ya heshima unapoenda kwenye sherehe.

Na kubwa kuliko usivae mavazi yaliyokufunika sana unapohudhuria katika tafrija hizo hapa namaanisha mavazi kama nikabu na mengine mengi yakujificha hayapendezi na katika yote jua kutofautisha nyakati.

Kuwa na mavazi ya faraja vazi la faraja ni lile vazi linalokupa uhuru unapolivaa hapa namaanisha lisiwe refu sana mpaka likapitiliza na lisikubane sana ukashindwa kutembea, vazi hili litakupa uhuru wa kusherekea na kuserebuka huku ukiwa mwenye furaha na amani uwapo ukumbini.

Fahamu rangi pendwa kulingana na rangi ya ngozi yako, siyo kila rangi inampendezaa mtu kulingana na ngozi ya mwili unapaswa ujue unapendezea rangi gani hichi ni kipengele muhimu sana cha kuzingatia katika monekano wako.

Unapaswa kufanya chaguo sahihi la nguo kulingana na rangi ya ngozi yako hii itakufanya upendeze na uvutie machoni pako na kwa wengine.

Jua umbo la mwili wako, kila mtu ana umbo lake awe mwanaume au mwanamke kwa kuzingatia umbo lako unapaswa kujua ni mitindo gani itakupendeza na itakupa mvuto zaidi kwa jinsi utakavyoamua kutoka kama mwalikwa wa siku husika.

Kwa kuzingatia mambo hayo mwalikwa ataweza kuchagua mavazi yanayofaa kwa sherehe husika, huku ukiwa mwenye kujiamini muda wote na mwenye furaha.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags