Mambo ya kuzingatia wakati wa kujiremba

Mambo ya kuzingatia wakati wa kujiremba

Habari msomaji wa fashion, Ni wiki nyingine tena tunakutaka ni kiamini kuwa u mzima wa afya tele na unaendelea na masomo yako pamoja na majukumu ya kulijenga taifa hili.

Leo hii tutaelezana na kujuzana mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kujiremba hasa kwa wanawake wanaopenda kwenda na wakati.

Nimeamua kuzungumza haya leo baada ya kuwaona wanawake wengi ujiremba bila kuzingatia mambo hayo muhimu jambo ambalo linalowafanya kuonekana kituko kwa wanaowatazama.

Jambo hilo la kujiremba bila kuzingatia mambo muhimu kwa sasa naona limekuwa tatizo kubwa kwetu sisi wanawake hasa kwa maharusi wanaofunga ndoa.

Ieleweke kuwa siku yako muhimu ni lazima upendeze lakini si kurembwa na vitu ambavyo vitafanya ubadirike sura yako na kuonekana kituko mbele ya jamii.

Basi tuyaangalie mambo hayo muhimu ambayo mwanamke akiyafanya yanazidisha urembo wake ambayo ni akizipendezesha kope zake, rangi ya mdomo, marashi, manukato au unyunyu kama wanavyoita vijana wa mjini.

Mambo mengine ni makeup ambayo itaendana na ngozi yako nayo pia usaidia kurembesha uso wako kikubwa kinachotakiwa ni kumpata mtu anaye weza kukuremba vizuri.

Kwa upande wa kope, tunajua zipo za  aina tofauti kwa urefu kinachotakiwa hapa ni kuzingatia aina gani itaweza kukupendeza ila nashauri si vizuri ukaweka kope ndefu sana.

Pia ni muhimu kuangalia rangi mbalimbali za kupaka kwenye kope ambazo zinatofautiana hivyo ni vyema kabla ya kupaka ukawasiliana na wataalamu wa mambo ya urembo kwa ushauri na siyo kukurupuka kwani unaweza kupaka rangi ambayo ukaonekana kituko mbele za watu.

Rangi ya mdomo nayo ni eneo lingine linalompendezesha mwanamke ila ukweli ni kwamba tunatofautiana sana midomo ambayo wazungu wanaita ‘lips’.

Kila mwanamke ana tofautiana midomo na mwingine kwahiyo hata rangi ya midomo nayo inakwenda sambamba na aina ya lips na rangi ya ngozi ya mwili aliyo nayo siyo unajisiriba rangi ya mdomo halafu unaonekana kituko.

Aidha natambua kuwa marashi au unyunyu ni muhimu sana kwa mwanamke lakini ni vyema nikaweka angalizo kuwa haipendezi kwa mwanamke nayepulizia manukato yanayonukia sana mpaka yakawakera wengine hivyo ni vyema wakajilipuzia marashi yenye staha yasiyokera.

Jambo lingine ni hili la Makeup, ni muhimu kupaka inayoendana na mwili wako na mtaalam anayejua hasa, usikubali mtu akakupaka makeup nyingi kiasi kwamba ikapoteza muonekano halisi wa sura yako.

Kama tutazingatia hayo wewe mwanamke unayesoma safu hii lazima utaonekana mrembo na wa kuvutia wakati wote. Tukutane tena wiki nyingine.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags