Mambo ya kuibua furaha katika mahusiano

Mambo Ya Kuibua Furaha Katika Mahusiano

Na Maria Basso

Mara nyingi huwa kama zimwi ambalo halikuli likakwisha, furaha katika ndoa ni kama njaa kwenye matumbo yetu huja na kuondoka mara kwa mara ..

Ungana nami katika dondoo hii nikikujuza mambo yanayoweza kuibua furaha iliyo kama nyoka mwenye miguu ya jongoo aliyekufa miaka kenda ..

1.Kubali kuyabeba madhaifu ya mwenza wako

Binadamu ni kama ngoma inayofutwa vumbi kila siku na kubwebwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kupigwa ili watu wacheze tunahitaji kuyabeba madhaifu ya wapendwa wetu ili maisha mengine yaendelee.

2.Usijaribu kufanya yote kwa pamoja

Kama vile kobe akimfuata mwenza wake kumng’ata sikio wakapumzike basi ndio hivyo ndoa hutaka tufanye ili mambo yaende jipe mda mwingi kukubali kubadilika na kufanya mambo kwa mikakati .

      3.Sikilizaneni

Kila aliye na pumzi basi hupenda kuwasilisha vitu na kusikilizwa kuna maana sana kumsikiliza mwenza wako hata kwenye maandiko matakatifu imeandikwa mtoto akimuomba babaye mkate  hatoweza kumpa jiwe atamsikiliza na kumpa atakacho.

          4.Mapenzi na furaha hutegemea muda

Mtoto huchukua miezi tisa sawa na siku 266 kutoka duniani ndivo hivyo mahusiano huwa furaha haiji kwa siku wala dakika inachukua mda kujengwa na kuitunza ili ndoa yako na mwenza wako kuwa yenye amani.

         5.Kuaminiana na heshima ni muhimu sana

kuwa na heshima na shukrani kwa yale mnayofanyiana katika  ndoa ni muhimu kuthamini kila mmoja anachokifanya kwa kutoa muda wake ni njia mojawapo ya kudumisha amani na furaha katika ndoa .

Yees!! Ni hayo tu machache ambayo nimekuandalia kwa siku ya leo hakikisha kama unayatakia mema mahusiano yako basi jitahidi sana kudumu kwenye mbinu hizi na utaenjoy mtu wangu!!.

Bila shaka unaweza kuongezea na ufundi wako bwana unaoujua wewe ili mambo yaweze kuwa bulbul kabisaa chukua hizo, ishi nazo utaona mabadiliko kwenye mahusiano yako.

Alaaa!! Kila la kheri mtu wangu uwanja ni wako sasa pambania kombeeee bye bye!!!.

 

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post