Mambo muhimu yakuzingatia kwa wanafunzi wa chuo

Mambo muhimu yakuzingatia kwa wanafunzi wa chuo

Niaje niaje, hivi chuo kinasemaje au ndo manapambania kombe, basi bwana kama kawaida yetu wazee wa kusababisha katika segment yetu ya unicorner, leo sasa tuko na mada ambayo sio tuu chuoni hadi kitaani itakusaidia.

Ukizungumza mambo muhimu mwanachuo wanatakiwa kuyazingatia yapo mengi, ila taratibu taratibu tutaelewana nini namaanisha, cha kukwambia tuu usiache kusoma magazine yetu inayotoka kila siku za Ijumaa ambayo imejaa Makala za kuelimisha na kuburudisha.

Nina furaha kubwa kupata fursa hii kuandika ujumbe huu kwenu. Hii ni kuhusu Elimu ya Juu na Maisha Halisi. Kama niwashaurivyo ninyi, nami pia najishauri.

Na haya ndo mambo ya msingi ya kuzingatia katika maisha yako ikiwa ni…

  • Unatakiwa kujua kuwa elimu ni msingi wa maisha.

Hili ni jambo muhimu sana la kutambua ni kwanini, lengo kubwa la wewe kuwa wanafunzi wa fani uliochagua ni kutengeneza msingi ili uweze kujenga maisha yako ya baadae.

Kwa msemo huu, ni maana kwamba elimu ni nyenzo mojawapo ya kutupa mwanga wa kufika sehemu furani. Kwa kusema hivyo nina maanisha kwamba elimu si kila kitu, bali ni nyenzo tu, inawezekana ukasoma mambo yanayohusu uhandisi wa majengo lakini ukajikuta umekuwa meneja wa mgahawa.

 Unaweza ukasomea fani ya mambo ya biashara ila ukajikuta ukaingia jeshi ukipiga kwata kila siku! Hayo yote yanawezekana na ukajiuliza kwanini ulisomea uhandisi lakini upo kwenye umeneja. Hapo ndipo inabidi utambue kwamba elimu uliyoisoma ni nyenzo tu na itabidi ujue jinsi ya kuitumia ili ifanikishe ujenzi wa nyumba nzima. Kumbuka kuwa msingi mbaya katika maisha kutaiporomosha nyumba unayoijenga.

  • Mfumo wa Elimu yetu si rafiki ambao unaweza kuturuhusu sisi kufanya mambo mengine kama vile ya kutuingizia kipato

Ukweli ni kwamba bado hatujifunzi vitu zaidi ya fani tunazosoma au kuwa sehemu ya wafanyakazi wasio rasmi. Kwa kusema hili, nina maanisha kuwa hudhuria matamasha ya kukujenga na kukufurahisha fanya bidii katika kutengeneza mifumo saidizi ambayo itakufanya hata mara baada ya kumaliza chuo utapata nafasi ya kujiendeleza au kupata sehemu ya kujishikiza mahala popote.

Ikiwezekana fanya biashara halali isiyovunja sheria za nchi. Jihudhurishe katika midahalo ya kimaendeleo, kiuchumi, ukuaji wa teknolojia na sayansi kwani midahalo hii itakupa mwanga kuhusu ni nini kinachotokea duniani katika uhalisia wenyewe.

Kwani ni kweli kuwa elimu na mitaala na vitabu tunavyovisoma wengi haitupi hali na picha halisi ya ukuaji wa dunia yetu katika mambo yote. Hivyo, "Jishughulishe” ukibweteka mwisho wa siku utarudisha mpira kwa golikipa.

  • Usiendekeze starehe zaidi.

Kuwa na kipimo sahihi katika kila unachokifanya (iwe katika masomo au starehe). Maisha yako yanategemeana kwa namna moja ama nyingine, ukizidisha upande mmoja unaua upande mwingine. Jiandae, jikabili na jitunze katika mambo yote.

Huwezi ukazidisha kitu kimoja na kukisahau kingine kwa maana kila kitu kina nafasi yake, jua jinsi ya kuikabili starehe yako unayoihusudu sana ili kufanya kila kitu kiwe katika mlinganyo stahiki ambao hautakufanya upoteze malengo yako.

  • Makundi unayochagua chuoni.

Makundi ya chuo kwa asilimia kubwa yanakufundisha wewe kwa maisha yako hata baada ya chuo. Hivyo hakikisha unakuwa na kundi ambalo linakujenga, linakupa motisha ya kwenda mbele, linakuonya na kukusikiliza.

Kama unataka kutengeneza umoja katika kazi, kundi ulilokuwa nalo linakutafsiri  vip mbele ya jamii ni nini hasa utakachokijenga maishani mwako. Kuna msemo wa kiingereza unaosema, "You choose your business partner at college."

  • Usiogope kufeli katika masomo.

Baadhi ya wanachuo wanaogopa na kuwa na hofu ya kutofikia malengo yako, ni kweli kuwa unapokuwa chuo, moja kati ya vitu vya msingi ni kufaulu masomo, Ila ukweli ni kwamba wengi wanapofika chuo ndipo wanapoweza kujipambanua ni nini wanachotaka yaani malengo wanayotaka kuyafikia.

Hivyo wengi wanahofu ya kufeli katika masomo kuliko kufeli katika malengo yao, tambua kuwa kufaulu masomo bila kuwa na malengo au kutofikia malengo yako ni sawa na kulipa nauli ya ndege kubwa halafu ukashindwa kusafiri kisa umekosa nauli ya kukutoa nyumbani mpaka uwanja wa ndege.

Yatafakari malengo yako na pia liangalie jambo unalolifanya chuoni kama kweli vinaendana na kama haviendani ni kheri ukatafuta njia mbadala ya kuyafikia malengo yako. "Usihofu katika jambo lolote, hofu ni kifo cha mtu aliyekosa maarifa."

ITAENDELEAAA…






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags