Ikiwa leo Oktoba 2, mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Naseeb Abdul 'Diamond' anasheherekea siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 35, ndani ya miaka hiyo msanii huyo tayari amefanya makubwa katika tasnia ya muziki nchini. Yaani unaweza kusema Diamond wa sasa siyo yule wa miaka mitano iliyopita.
Matamanio na mafanikio ya Diamond
Nyimbo/wimbo wake kupigwa na mataifa zaidi ya 20
Diamond ambaye ndiye Mtanzania mwenye wafuasi wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii, akiwa na 'views' zaidi ya bilioni 2.6 na wafuasi milioni 9.2 kwenye mtandao wa YouTube,kati ya mafanikio ambayo amekuwa akijivunia ni wimbo wake ‘Komasava remix’ aliyomshirikisha Jason Derulo, Khalil Harisson na Chley.
Wimbo huo ambao uliachiwa rasmi miezi miwili iliyopita hadi sasa umetazamwa zaidi ya mara milioni 21 katika mtandao wa YouTube huku challenge yake ikichezwa na mastaa mbalimbali duniani akiwemo Chris Brown.
Mbali na wimbo huo kuwakosha wadau wa muziki, siku chache baada ya kuachiwa kwake ulifanikiwa kuingia katika chati za Billboard na kushika nafasi ya 39 katika Kipengele cha Afrobeats Songs Top 50.
Kunyakua tuzo kubwa duniani
Msanii huyo amewahi kupata tuzo kubwa duniani kama vile MTV barani Ulaya (MTV EMA), MTV, AFRIMMA na nyinginezo huku kwa sasa lengo lake likiwa kushinda tuzo kubwa za muziki kutoka Marekani ‘Grammy’.
Kuwa tajiri namba moja duniani
Mbali na hayo msanii huyo hivi karibuni alieleza kuhusiana na ndoto yake ya kuzifikia ‘levo’ za watu matajiri zaidi duniani akiwemo; Elon Musk, Bernard Arnault, Bill Gates, Aliko Dangote na Jeff Bezos.
“Ndoto yangu kubwa katika maisha ni kuwa tajiri namba moja duniani, ndiyo ndoto yangu na ninakuthibitishia kwamba nitakuwa tajiri namba moja duniani. Kwa sababu kwangu mimi naamini kila kitu kinawezekana, na ninawahakikishia kuwa Mtanzania nitakayewakilisha taifa kwa kuwa tajiri namba moja duniani," alisema Diamond mwezi mmoja uliyopita
Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ alizaliwa Oktoba 2, 1989 mkoani Kigoma na ameipeperusha bendera ya Tanzania kupitia ngoma zake kama ‘Komasava’, ‘Shu’, ‘My Number one’, Marry You’, ‘African Beauty’ na nyinginezo.
Leave a Reply