Mama wa Maguire awatolea povu wanao mshambulia mwanaye

Mama wa Maguire awatolea povu wanao mshambulia mwanaye

Mama mzazi wa mchezaji wa ‘klabu’ Man United, Harry Maguire amemkingia kifua mwanaye baada ya nyota huyo raia wa England kukosolewa vikali baada ya kujifunga wakati wa mchezo wa ‘klabu’ ya England dhidi ya Scotland.

Kupitia ujumbe mzito na wenye hisia kwenye mitandao ya kijamii, Zoe Maguire mbaye ni mama wa mchezaji huyo  ametoa wito kwa mashabiki wa England, wachambuzi na vyombo vya habari kumpumzisha mwanaye.

Ameeleza yeye kama mama akiona mwanaye anakashifiwa mitandaoni na baadhi ya mashabiki, wachambuzi na waandishi wa habari hatakubali.

Mama huyo aliendelea kusema katika ulimwengu wa ‘soka’ kuna kupanda na kushuka lakini anachopokea mwanaye anadai kimeenda mbali zaidi ya maswala ya mpira wa miguu.

Mama alikanusha kwa wale waliyomwambia mchezaji huyo kama alirukwa na akili na kusema mtoto wake akili zake ni timamu na hawezi kujifunga kwa kudhamiria akieleza kuwa amesikitishwa na hatamani unyanyasaji wa aina hiyo uje umtokee mtu yeyote.

Ikumbukwe Maguire alijifunga dakika ya 67 muda mfupi baada ya kuchukua nafasi ya Marc Guehi mwanzoni mwa kipindi cha pili cha mchezo kati ya Scotland dhidi ya England ambapo England ilishinda 3-1 kwa mabao ya Philip Fiden, Jude Bellingham na Harry Kane.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags