Mama mzazi wa MJ apata urithi wake

Mama mzazi wa MJ apata urithi wake

Baada ya mama mzazi wa marehemu mfalme wa Pop Michael Jackson, Katherine Jackson (93) kukata rufaa dhidi ya wasimamizi wa mali za MJ, hatimaye wasimamizi wa mali hizo wamemkabidhi Bi Katherine kiasi cha dola 55 milioni sawa na tsh 141 bilioni ikiwa ni sehemu ya mali za mwanaye.

Kwa mujibu wa #Tmz imeeleza kuwa siku jana wasimamizi wa mali za MJ walifika ofisini kwao na kuwaonesha hati ya makabithiano ya mali hizo.

Ambapo Katherine Jackson amekabidhiwa kiasi hicho cha pesa ambacho kimekusanywa ndani ya miaka 15 tangu mwanaye MJ alipofariki Juni mwaka 2009.

Ikumbukwe kuwa siku ya Jana Machi 21, mtoto wa mwisho wa MJ, Bigi Jackson maarufu kama MJ Blanket (22) aliwasilisha ombi katika mahakama nchini humo kutomruhusu bibi yake kutumia pesa za MJ kwa ajili ya kukata rufaa kutokana na kutoona kama kesi hiyo itashinda.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags