Mama Kama Mtoto

Mama Kama Mtoto


Baada ya mtoto wa Kim Kardashian, North West kushambuliwa kupitia mitandao ya kijamii akifananishwa na kifaranga kupitia vazi lake la manyoa, sasa ni zamu ya mama yake kuzodolewa mitandaoni baada ya kuiga vazi hilo.

Mfanyabiashara huyo anayemiliki chapa ya SKIMS alishare picha akiwa ameiga vazi la mwanaye North alilolivaa katika tamasha la ‘The Lion King’ ambapo mashabiki waliibuka upande wa ‘komenti’ na kumrushia maneno kwa kudai kuwa aacha kumuiga mtoto wake na atafute ubunifu wake.

Aidha baadhi ya mashabiki pia walikasirishwa na picha hizo wakiamini kwamba Kim alikuwa mbinafsi, ambapo mmoja wa wadau aliandika ‘Hukuweza kumruhusu binti yako apate muda ilibidi uivae pia’.

Kumbuka kuwa North West ni mtoto wa Kim Kardashian na aliyekuwa mumewe Kanye West.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post