Maluma arushiwa simu na shabiki  wakati akitumbuza

Maluma arushiwa simu na shabiki wakati akitumbuza

Mwanamuziki kutoka nchini #Colombia, #Maluma naye akutana na vioja vya mashabiki kurushia vitu wasanii wakiwa jukwaani wanatumbuiza.

Awamu hii Maluma arushiwa simu na shabiki akiwa jukwaani anatumbuiza kwenye tamasha, San Antonio.

Shabiki huyo katikati ya show alisogea hadi mstari wa mbele karibu kabisa na jukwaa na kumtupia Maluma simu ya mkononi.

Kwa bahati nzuri ilimpata kwenye kiwiliwili hivyo haikumpata sehemu yoyote ya hatari wala kumletea matatizo. Kutokana na hilo nyota huyo alionekana kumkanya shabiki huyo asirudie tena kitendo alichofanya.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags