Malkia Letizia ndani ya ‘fainali’ kombe la dunia la wanawake

Malkia Letizia ndani ya ‘fainali’ kombe la dunia la wanawake

Malkia Letizia kutoka nchini Hispania anatarajia kusafiri kuelekea Austaria kwa ajili ya kutizama ‘mechi’ ya fainali za kombe la Dunia la wanawake. Ambapo ‘mechi’ hiyo itakuwa kati ya England na Hispania.

Taarifa hiyo imetolewa na Shirikisho la Soka la nchini Hispania na kueleza kuwa Malkia Letizia atahudhuria ‘mechi’ hiyo na binti yake Infanta Sofia (16). Kutokana na kutingwa na shughuli zingine Mfalme Felipe wa Hispania hatoweza kuhudhuria.

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho kwa ‘Timu’ ya Taifa ya Soka ya England kuingia katika Fainali za Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1966, ‘mechi’ hiyo iliyochezwa Wembley ilihudhuriwa na Malkia Elizabeth II, ‘timu’ hiyo iliifunga West Germany ‘goli’ 4 kwa 2.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags