Mali za Tekashi zatakiwa kupigwa mnada kulipa fidia

Mali za Tekashi zatakiwa kupigwa mnada kulipa fidia

Rapa kutoka nchini #Marekani, #Tekashi6ix9ine atalazimika kuuza mali zake za thamani ili kulipa faini ya dola 9.8 milioni, ambazo ni zaidi ya tsh 24 bilioni, kufuatia uamuzi wa jaji wa Florida katika kesi ya kumpiga kichwani na chupa Alexis Salaberrios katika klabu ya ‘strip’ mwaka 2021.

Jaji Robert T. Watson amethibitisha uamuzi huo kwa rapa huyo baada ya kushindwa kufika Mahakamani kupinga uamuzi huo mwezi Julai mwaka huu.

Mali zinazotakiwa kuuzwa ni pamoja na gari aina ya Rolls-Royce, jumba lake la kifahari la Florida na vitu vingine vya bei ghali ambavyo vinaweza kuuzwa kwa mnada ili kulipa fidia ya dola milioni 9.825.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags