Makalla: Mgao wa maji Dar umeisha

Makalla: Mgao wa maji Dar umeisha

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amesema mgao wa maji katika mkoa wa dar es salaam umefika mwisho mara baada ya kuongezeka kwa maji katika kituo cha Maji cha Ruvu chini kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni.

RC Makalla ameyasema hayo leo Novemba 25 katika ziara ya kukagua chanzo cha maji cha Ruvu chini na kusema kuwa kwa sasa maji yapo ya kutosha isipokuwa bado DAWASA wanahakikisha wanaboresha miundombinu ili maji yafike kwa kila mwananchi kwa wakati.

Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu wa Dawasa Cyprian Luhemeja amesema kama wasimamizi wakuu wa maji wamepita kipindi kigumu sana kutokana na ukame uliokuwepo mkoani Dar es salaam na amewashukuru viongozi wa dini mbalimbali kwani kilichotokea ni kama miujiza kwani mvua zimenyesha kwa wingi.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post