Makabila amewasili kituo cha polisi Oysterbay

Makabila amewasili kituo cha polisi Oysterbay

Baada ya kuzuka tetesi kuhusina na mwanamuziki wa Singeli nchini Dulla Makabila kufunguliwa mashitaka na aliyekuwa msemaji wa ‘klabu’ ya Yanga Haji Manara na mchumba wake Zaiylissa, hatimaye Makabila tayari amewasili Kituo cha Polisi Oysterbay kwa ajili ya kusikiliza wito huo.

Dulla Makabila na Haji Manara wameingia katika bifu zito baada ya Makabila kuachia ngoma iliyodaiwa kuwa amemuimbia aliyekuwa mke wake wa zamani Zaiylissa ambaye kwa sasa ni mchumba wa Manara.

Haji Manara alimchumbia Zaiylissa siku ya Alhamis Januari 18, ikiwa ni siku ya kuzaliwa ya Manara, ambapo baada ya kupita kwa tukio hilo Makabila aliachia singeli iitwayo ‘Furahi’ ambayo mpaka kufikia sasa inazaidi ya watazamaji Laki tano huku ikiendelea kushika namba moja trending kupitia mtandao wa YouTube.

Kabla ya kuvishwa pete na Manara, Zaiylissa aliwahi kufunga ndoa na Dulla Makabila May 2023 na kuachana Julai mwaka huo huo, wakitimiza mwezi mmoja tuu ndani ya ndoa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags