Majukwaa ya muziki yadaiwa kufungia Album ya Tory Lanez

Majukwaa ya muziki yadaiwa kufungia Album ya Tory Lanez

Wakili wa rapa Tory Lanez, Moe Gangat ameyalalamikia majukwaa ya muziki kuficha Album mpya ya 'Peterson' kutoka kwa msanii huyo akidai kuwa hawataki iingie kwenye trend.

Wakili huyo amelalamikia majukwaa ya muziki kama vile Apple Music na Spotify akisema maudhui ya album hiyo yamefichwa lakini pia nyimbo zake zimetolewa kwenye trend.

Album hiyo ya Peterson kutoka kwa Tory lanez iliachiwa Ijumaa ya Machi 7, 2025 ikiwa na jumla ya nyimbo 20 ambazo zimeandaliwa na kukamilishwa na rapa huyo akiwa Gerezani akitumikia kifungo cha miaka 10 baada ya kupatwa na hatia ya kumpiga risasi rapa Megan Thee Stallion mwaka 2020.

Aidha, Rapa Tory kupitia wimbo wake wa Free Tory unaopatikana kwenye album yake mpya amemshukuru msanii Chriss Brown kwa msaada wake wa fedha za kuendeshea mashataka ya kesi yake baada ya marafiki na watu maarufu kumzimia simu akiwa kwenye janga hilo.

"Sikuweza kufikia pesa zangu. Nilichoshwa na wakili wangu alitaka malipo yake kuniwakilisha kwa ajili ya kukata rufaa. nikaanza kuwatafuta marafiki zangu wote wa rap, marafiki zangu watu mashuhuri, na hakuna mtu aliyekuwepo

"Waliona kama vile nimeshakufa lakini Chris Brown siwezi kukusahau. Alinipa pesa tu. Akasema, angalia kaka ukifika nje nitafute. Natumai utatoka gerezani," ameimba Tory.

Tory na Chriss wana uhusiano wa muda mrefu katika kazi wakiwa wameshirikiana katika nyimbo kama vile 'Lurkin,' 'Feel,' 'The Take,' na 'Drifting.'






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags