Majina ya mastaa yaliyochafuliwa kufuatia kesi za Diddy

Majina ya mastaa yaliyochafuliwa kufuatia kesi za Diddy

Ikiwa zimetimia siku 14 tangu mkali wa Hip Hop Sean Combs 'Diddy' kuishi katika kuta za gereza hatari zaidi Marekani la Metropolitan, kwa upande wa mastaa aliyowaacha uraini majina yao yamekuwa yakitajwa kwa namna Fulani katika kesi zinazomkabili

Katika mitandao ya kijamii kumekuwa na stori mbalimbali kuhusiana na baadhi ya mastaa ambao waliokuwa karibu na rapa huyo kuhusishwa moja kwa moja kwenye kesi za Diddy moja wapo ikiwa ni kuhusishwa kwenye biashara ya ngono.

Usher Raymond
Usher na Combs walifahamiana mwaka 1994, akiwa na umri wa miaka 15 wakati alipokuwa akijitafuta kimuziki na alipelekwa kuishi nyumbani kwa Combs huko Scarsdale, New York mpaka pale alipojipata.

Jina la Usher limekuwa likitajwa katika mitandao ya kijamii kuwa huenda akawa anahusika kwa namna Fulani kuhusiana na maswala biashara za ngono zilizokuwa zikiendelea nyumbani kwa Diddy.

Hata hivyo baada ya Combs kukamatwa msanii huyo, kupitia akaunti ya Usher ya X amefuta picha zote ambazo aliposti akiwa na Diddy jambo ambalo lilizua taharuki kwa mashabiki, ambapo badae Usher alitoa taarifa kuwa akaunti hiyo ilidukuliwa.

Justin Bieber
Akiwa na miaka 13 Bieber alikutana na Combs kwa mara ya kwanza baada ya Usher kumtambulisha msanii huyo mchanga ambaye alitamani kutoka kimuziki, ambapo safari ya kuwa karibu na Diddy ilianzia hapo huku akidaiwa kuhudhuria kwenye Party za Puff zilizojaa kila aina ya uchafu akiwa na umri mdogo.

Baada ya Usher kumtambulisha Bieber kwa Diddy mitandao ya kijamii imeibuka ikimshambulia Usher kwanini alimpeleka Bieber kwa Combs angali alikuwa akijua yanayokenda kumkuta. Jina la Bieber limekuwa likichafuliwa na kutajwa kuhusika kwenye mambo ya ngono huku mashabiki wakimuonea huruma kutokana na kujihusisha na masuala hayo akiwa na umri mdogo.

Hata hivyo masaa machache baada ya Diddy kukamatwa Daily Mail iliripoti kuwa Bieber ambaye alikuwa akimuangalia Diddy kama Role Model wake anajutia ukaribu alioweka na rapa huyo wakati anaaza kufanya muziki akiwa na miaka 14 huku ikidaiwa kuwa toka Diddy akamatwe Bieber amejifungia ndani na kusitisha mawasiliano na watu wengine zaidi ya familia yake.

Meek Mill
Mill alianza urafiki na Diddy walipokutaka katika sherehe za ugawaji wa tuzo za Grammy, na baadae wakawa wakionekana pamoja mara nyingi ambapo Mill alishirikishwa kwenye ngoma ya Diddy iitwayo ‘I Want The Love’ huku Combs akiwepo kwenye wimbo wa Mill ‘Cold Hearted’.

Urafiki wa wawili hao ulizuka kwa gafra jambo ambalo mashabiki wamekuwa wakilikumbushia baada ya Diddy kukamatwa ambapo wanadai kuwa Mill huenda naye akawa mfuasi wa Combs kwenye masuala ya biashara za zongo.

Kufuatia na minong’ono hiyo siku chache zilizopita Mill kupitia ukurasa wake wa X alitoa taarifa kuwa amepanga kuwalipa wapelelezi ili kuwafahamu watu wanaolihusisha jina lake na kesi za Combs.

Meek ameeleza kuwa yupo tayari kutoa kiasi cha dola 100,000 sawa Sh 273 milioni kwa wapelelezi kufanya uchunguzi watu wanaolihushisha jina lake katika kesi zinazomkabili Diddy.

Burna Boy
Kwa upande wa Bara la Afrika msanii mkubwa ambaye jina lake limekuwa likitajwa na kuhusishwa kwenye kesi za Diddy ni mkali wa Afrobeat Burna Boy ambaye aliwahi kufika nyumbani kwa Combs.

Burna alikutana na Diddy kwa mara ya kwanza mwaka 2021 ambapo, Combs alimsaidia Burna kutengeneza album yake liyoshinda tuzo ya Grammy, ‘Twice as Tall’, kwa njia ya Zoom, ambapo kufutia na matukio hayo mashabiki wamekuwa wakimuhusisha mkali huyo wa Afrobeat na masuala ya ngono. Hata hivyo Burna hajatoa tamko lolote mpaka kufikia sasa.

Diddy alikamatwa Jumatatu Septemba 16, na kuzuiwa katika gereza linaloitwa ‘The Metropolitan Detention Center (MDC) kwa tuhuma za ulaghai wa kingono na usafirishaji wa binadamu ili kujihusisha na biashara hiyo ya ngono.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags