Maisha ya mtaani baada ya kumaliza vyuo vikuu

Maisha ya mtaani baada ya kumaliza vyuo vikuu

Na Magreth Bavuma

Ouyah!! wanangu wa moyoni eeeeh mambo ni gani, it’s another blessed week karibu nyumbani “unicorner” Tuone ni nini kona yetu imebeba, dua yetu ni ile ile M/mungu atuepushe na kutokufanikiwa, let’s go......

Ukiwauliza baadhi ya wanavyuo juu ya ile kauli ya “chuo bata” wanaweza wakawa na majibu sahihi sasa baada ya kuingia na kuona kumbe yaliyomo yamo, na utagundua kwamba everyone’s got their own university experience, mpaka kufikia mwisho wa mwezi huu, baadhi ya wanavyuo watakua wanahitimu na kuingia katika ulimwengu mpya wa maisha ya mtaani.

Yaaani ndo ileeee hakuna boom, na home wanaweza wakaanza kukukazia ki aina. Wakati huu unaweza kuleta hofu na wasiwasi, pamoja na yote ni muhimu kuwa na mwongozo ambao utawapa mori na kuwawezesha kujiamini wanapoelekea kwenye hatua mpya ya maisha yao.

Kwa pamoja tucheki mambo muhimu ya kuzingatia na hatua za kuchukua ili kuwa na mwelekeo imara na kujiondoa hofu ya maisha ya kitaa.

Kujenga mtandao wa kazi na ushirikiano (Networking)

Moja ya mambo muhimu unaporudi kitaa ni kujenga mtandao wa kazi na ushirikiano, tafuta fursa za kujiunga na makongamano, semina, na mikutano inayohusiana na eneo lako la taaluma.

Pia, tumia mitandao ya kijamii na tovuti za kazi kuanza kuwasiliana na wataalamu katika sekta unayotaka kufanya kazi. Kwa kuwa na mtandao mzuri, utapata fursa za ajira na ushauri wa kitaalam ambao utakuwezesha kufanikiwa katika maisha ya mtaani.

Kuendelea na mafunzo na kujifunza

Kumaliza masomo ya darasani haimaanishi uache kujifunza, kwa kuwa  kuendelea kujifunza na kuboresha ujuzi wako ni jambo muhimu katika kukabiliana na maisha ya mtaani.

Jiunge na kozi za mafunzo, semina, au programu za mafunzo ya kuendeleza ujuzi wako katika eneo lako la taaluma. Pia, fanya utafiti kuhusu soko la ajira na mwenendo wa kazi katika sekta unayopenda. Kuwa na ujuzi na maarifa yanayokidhi mahitaji ya soko la ajira kutakupa ujasiri na fursa zaidi katika maisha ya mtaani.

Kuwa na mipango na malengo

Siku zote kupiga hatua hakuji kama bahati nasibu lazima ujiwekee mipango na malengo na uhakikishe unatembea katika njia sahihi inayoendana na mipango na malengo yako hii ni muhimu na itakusaidia katika kujiondoa hofu na kuwa na mwongozo katika maisha ya mtaani.

Jiwekee malengo ya muda mfupi na mrefu na panga njia za kufikia malengo hayo, lakini usisahau kwamba kabla ya mbili kuna moja na mtaani kuna either kuajiriwa au kujiajiri ni vizuri kuwa na mbadala wa kila lengo au mpango yaani alternatives ili upande mmoja uki bonce basi unatumia upande mwingine.

Fanya orodha ya hatua za kuchukua na ratiba ya kutekeleza malengo yako itakusaidiaa pia katika kujiamini na kuwa na mwelekeo wakati unakabiliana na changamoto za maisha ya kitaa.

Kujitayarisha kifedha

Ukweli ni kwamba kitaa kinataka pesa na yamkini utofauti wa maisha unaanza baada ya kuingia mtaani na matumizi yanaweza kubadilika kadri siku zinavyozidi kusonga baadhi yetu tunaweza kuwa hatuna utaratibu wa ku save pesa wala kuwa na matumizi mazuri, lakini kujiandaa kifedha ni muhimu katika kujiondoa hofu ya maisha ya kitaa.

Jitahidi kuwa na mpango mzuri wa bajeti, kuweka akiba, na kujifunza jinsi ya kusimamia pesa yako vyema. Pia, fanya utafiti kuhusu fursa za mikopo na ufadhili unaopatikana kwa wajasiriamali na wafanyakazi wa kujitegemea. Bado hujachelewa Kuwa na msingi thabiti wa kifedha kutakupa uhuru na usalama katika maisha ya kitaani.

Kuwa na mawazo chanya na kujithamini (positive minded)

Hofu inaanzia kwako hivyo ni wewe kupambana nayo na ili kufanikiwa katika hilo lazima uwe positive minded about everything you do, kuwa na mawazo chanya na kujithamini itakusaidia kujiamini na kujiondoa hofu ya maisha ya kitaa.

Jitahidi kuwa na mtazamo wa ukuaji na kuamini katika uwezo wako wa kufanikiwa, jipongeze kwa mafanikio madogo na kumbuka thamani yako binafsi kuwa na tabia ya kujithamini na kujiheshimu kutakusaidia kuvuka vizuizi na kufanikiwa katika kuona kwamba street life is possible.

Yote kwa yote, kujiandaa na kujiweka tayari kwa maisha ya kitaa ni muhimu sana, wanavyuo wanaohitimu wanaweza kupambana na hofu na kuwa na ujasiri katika kuingia kwenye ulimwengu mpya wa maisha.

Kumbuka, maisha ya mtaani yana fursa nyingi na uwezo wa kukuletea mafanikio makubwa. They say that street life ain’t easy but you got this, Hakikisha unamtanguliza Mungu, unazingatia nguvu zako, penda kile unachofanya, na kuwa tayari kuchukua hatua.

Kiufupi usiingie mtaani kinyonge you have that kinda ability and energy you can do this go and make yourself proud. Na sisi tunawatakia kila la kheri na kila jema likawe upande wenu.

Naam! wanangu eeh tuendelee ama tusiendelee ahahaha mi naona kwa leo tuishie zetu hapa, tukutane tena wiki ijayo kona yetu ile ile “unicorner” asanteni sana kwa kuendelea kunipa shavu kiukweli sapoti yenu ndio inaniweka mjini Mungu awaweke bana kwa ajili yangu until next time tchaaaaoooooo!!!!!!!!!!!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags