Maguire atishia kuondoka Man United

Maguire atishia kuondoka Man United

‘Beki’ wa kati wa #ManchesterUnited, #HarryMaguire amedai kuwa kama ataendelea kupata nafasi ndogo ya kucheza chini ya ‘Kocha’ Erik ten Hag basi atafikiria kuondoka ifikapo Januari 2024.

Maguire ambaye alitoa 'asisti' ya ‘goli’ la ushindi ‘mechi’ iliyopita dhidi ya #Brentford, amesema  kuwa hawezi kubaki ‘klabuni’ hapo akiwa anacheza mara moja kila mwezi na hali hiyo ikiendelea kuwa hivyo atazungumza na ‘klabu’ hiyo kwa sababu anaamini uwezo wake na anataka kuonesha ili awe sehemu ya wachezaji muhimu katika ‘timu’ hiyo.

Ikumbukwe Maguire awali alikuwa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza kutokana na walinzi wa Man United kuwa majeruhi, wakiwemo Rafael Varane, Lisandro Martinez, Aaron Wan-Bissaka, Tyrell Malacia, Luke Shaw na Sergio Reguilon.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags