Mafuriko yasomba miili kutoka kwenye makaburi

Mafuriko yasomba miili kutoka kwenye makaburi

Baadhi ya miili kutoka makaburi ya kingo za mto Umbeluze karibu na mji mkuu wa Msumbiji, Maputo, imesombwa na mafuriko na kuenea katika makazi ya watu na mashamba.

Vituo vya televisheni vilionesha madhara ya maji yaliyochafuka ambayo yalifurika vitongoji vingi katika wilaya ya Boane, takribani kilomita 25 kusini magharibi mwa mji mkuu, na kwingineko.

Miili iliyotawanyika inaripotiwa kuhatarisha afya ya umma. Wanajamii walitumia wikiendi kukusanya maiti.

Kimbunga cha kitropiki Freddy kilipiga nchini humo siku ya Ijumaa na kusababisha mafuriko makubwa katika eneo lote.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags