Mafanikio ya Sadio Mane katika soka

Mafanikio ya Sadio Mane katika soka

It’s furahidayyyyyy! Nyie ama kweli siku hazigandi, ramadhani ndo hiyooo inaenda kuishia zake, basi bwana leo katika segment yetu ya burudani na mishezo tumekusogezea mwanasoka kutoka Afrika anaeumiza vichwa vya timu nyingi barani Ulaya kutokana na kiwango chake, huyu ni Sadio Mane.

Alizaliwa Aprili, 10,  1992 katika kijiji cha Bambali nchini Senegal. Miasha yake ya utotoni yana mikasa mingi ya kusikitisha kwa sababu alishindwa kwenda hata shule kwa wakati huo kutokana na ugumu wa maisha wa familia yao na katika moja ya mahojiano Mane aliweka wazi kwamba familia yao ilikuwa na watoto wengi kiasi cha wazazi wake kushindwa kumpeleka shule.

Hiyo ikasabisha muda mwingi Mane acheze mpira kwa sababu ndio kazi pekee aliyokuwa anaiweza kuifanya pale alipokuwa akimka kila siku asubuhi.

Mane anasimulia kwamba familia yake ni waumini wa dini ya kiislamu hivyo ndoto ya wazazi wake ilikuwa ni kuona siku moja amekuwa shee mkubwa hivyo kuna nyakati walikuwa wakimzuia hadi kucheza mpira.

Ilipofika muda wa kutaka kwenda mjini kuendeleza kipaji chake cha soka Mane anadai ilikuwa ni ngumu kuruhusiwa licha ya wanakijiji wote kuamini kwamba anajua wazazi wake walikuwa hawataki acheze soka.

Baada ya malumbano ya muda mrefu Mane aliruhusiwa kwenda mjini na pesa ya nauli ilipatikana baada ya wazazi wake kuuza mazao yote waliyoyavuna.

Baada ya kufika Dakar ambao ni mji mkuu wa Senegal, Mane alijaribu kwenda kufanya majaribio kwenye timu kadhaa na akafanikiwa kuchagulia akacheza hapo kwa misimu miwili kabla ya maskauti kutoka Ufaransa kumuona na kumpa nafasi ya kwenda Ufaransa akitokea Akademi ya Generation Foot na alipofika Ufaransa alijiunga na timu za vijana za Metz na  hapo akaanza kucheza timu ya wakubwa akiwa na umri wa miaka 15 tu.

Baada ya kiwango bora na Metz alijiunga na RB Salzburg katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2012 kwa ada ya Euro 5 milioni.

Alidumu hapo hadi mwaka 2014 kisha akatua rasmi kwenye Ligi Kuu England akiichezea Southampton ambako alikaa hadi 2016 kisha akajiunga na Liverpool kwa dau la Euro 41 milioni.

Alidumu hadi mwaka jana na akaondoka baada ya Liverpool kugoma kumuongeza mshahara, hivyo akaachana nao na kwa sasa anaichezea Munich ambayo inamlipa Pauni 350,000 kwa wiki inayofikia milioni 700 kwa pesa za kibongo.

REKODI NA MAFANIKO YAKE

  • Aliisaidia Liverpool kwa kushinda taji la Ligi Kuu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 msimu wa...

 

  • Oktoba 2021, alifunga bao lake la 100 la Ligi Kuu, na akawa mchezaji watatu kutoka Afrika.
  • Pia Mane ni mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Senegal.
  • Ameiwakilisha Senegal kwenye michuano ya

Olimpiki ya 2012.

  • Ameichezea Senegal mara nne kwenye michuano ya AFCON mwaka 2015, 2017, 2019 na 2021 na akawa mchezaji bora wa michiano hiyo kwa mwaka 2021.
  • Mfungaji bora Ligi Kuu England msimu 2018-19.
  • Mchezaji bora wa Afrika mwaka 2019,2022.
  • Mataji ya michiano yote -12

UTAJIRI WAKE

Mane ambaye kwa sasa ana umri wa miaka  31, ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 25 milioni, sehemu kubwa ya kipato chake  ni mshahara anaolipwa na Munich wa Pauni 350,000 kwa wiki sambamba na madili mengine ya nje ya uwanja.

Madili ya nje ya uwanja ambayo staa huyu anayapiga ni yale ya ubalozi wa kampuni mbali mbali ikiwa pamoja na ubalozi wa  Western Union,Utalii wa Indonesia na New Balance.

MSAADA KWA JAMII

Mane ni miongoni mwa wachezaji waliolelewa kwenye mazingira magumu sana, hivyo amekuwa akijitahidi sana kusaidia jamii.

Mwaka, 2019 alitumia kiasi kisichopungua Euro 270,000 kwa ajili ya kujenga shule kwenye kijiji cha Bambali apozaliwa na kulelewa,

Mbali ya shule staa huyu pia aligharamia ujenzi wa Hospitali kijijini  hapo na mara kadhaa amekuwa akipeleka misaada ya chakula, pesa na vifaa vya michezo kwa familia za eneo hilo.

Katika kipindi cha janga la Uviko, Mane alitoa msaada wa Pauni 41,000 kwenda mamlaka za afya nchini Senegal.


UHUSIANO

Anadaiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwandishi wa habari Melissa Reddy anayefanya kazi kwenye shirika la utangazaji nchini England BBC.

Haijawahi kuthibitika na watu wamekuwa wakihisi kwa sababu amekuwa akionekana naye mara nyingi kwenye mahojiano na huwa kuna viashiria kwamba wawili hao wapo kwenye uhusiano. Mane huwa hapendi kuweka wazi maisha yake binafsi.

 NYUMBA

Mara nyingi huwa hapendi kuweka mambo yake wazi, hivyo haijajulikana  ana jumla ya nyumba ngapi, lakini nyumba inayotambulika ni ile iliyopo  Allerton kusini mwa Jiji la Liverpool na ina thamani ya Dola 2 milioni.

NDINGA

Ana magari kibao yenye thamani ya Dola 665,000 yote kwa pamoja.

Mercedes G63 AMG-dola 200,000

Bentley Continental GT - dola 200,00

Audi RS7-dola 120,000

Range Rover Evoque-dola 45,000






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags