Madonna atoka ICU

Madonna atoka ICU

Mwanamuziki na Muigizaji maarufu Marekani, Madonna mwenye umri wa miaka 64 ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kuwepo kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa siku kadhaa.

Taarifa za kuugua kwake zilitolewa na Meneja wake wa muda mrefu Guy Oseary ambaye alithibitisha kuwa msanii huyo alipatwa na maambukizi makali ya bakteria na kupelekea kukimbizwa hospitali jumamosi iliyopita.

Msanii huyo alikuwa katika hatua za mwisho za mazoezi kwa ajili ya tour yake ya miezi 7 ya dunia ambayo ilipangwa kuanzia Canada mwezi Julai na kuendelea katika miji 45 katika nchi mbalimbali, akiadhimisha miaka 40 ya msanii huyo.

Mtaalamu wa afya ameeleza kuwa ugonjwa alioupata Madonna ulikuwa mbaya, ikiwa mgonjwa hapati matibabu sahihi na mapema huweza kupelekea viungo vyake kufeli na hata kifo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags