Habari msomaji wetu ni siku nyingine tena tunakutaka hapa nikiamini u mzima wa fanya tele na unaendelea vema na majukumu yako ya kila siku.
Leo katika dondoo za fashion napenda kuwajuza juu ya madhara ya kiafya yanayotokana na uvaaji wa wigi na usukaji wa nywele za bandikia kwa wanawake.
Wigi au usukaji wa nywele za bandia ufanywa na kinamama wengi hasa wale wenye asili ya Afrika au wamarekani wa asili ya Afrika kwa lengo la kuongeza urembo, mvuto na kuonekana maridadi wakati wote.
Hata hivyo siku hizi warembo hasa wanaoshiriki katika mashindano ya urembo hujaribu kurefusha nywele zao ili kuwa na viwango na aina za mitindo ya ughaibuni.
Wataalamu wa afya wanatueleza kwamba uvaaji wa wingi au nywele za bandia waweza kukusababishia matatizo yafuatayo endapo malighafi au kemikali zilizotumika kutengeneza wigi hilo zitasisimua mfumo wa kinga ya mwili wa mvaaji.
Wataalamu hao wanasema moja ya madhara yanayotokana na kuvaa wigi au kusukia nywele za bandia ni kupata mba kichwani, hiyo inatokana na kukosekana kwa hewa ya kutosha ya oksijeni katika ngozi ya kichwa na katika tishu za shina la nywele.
Pia unaweza kunyonyoka nywele, hata kama una nywele nzuri zenye afya kama utachagua kuvaa wigi au kusuka nywele za bandia kichwani mwako bila kufuata taratibu za kuhakikisha kuwa nywele zako ni safi lazima utanyonyoka nywele tu.
Madhara mengine wanatueleza kuwa ni maumivu ya kichwa, ambapo wanafafanua kuwa wigi au usukaji wa nywele bandia unaweza kusababishia maumivu makali ya kichwa, kwani wigi lililo dogo husababisha mnkandamizo kichwani na kuleta maumivu makali ya kichwa mara kwa mara.
Aidha harufu mbaya huweza kujitokeza endapo mba na jasho vitachanganyikana na hali hiyo hupelekea uwepo wa bacteria au fangasi na kusababisha muwasho mkali, hii yaweza kumkosesha raha mvaaji wigi na msukaji wa nywele za bandia hasa pale anapokuwa katika mkusanyiko wa watu.
Ushauri
Wataalamu hao wameeleza kuwa si vema kulazimisha kuvaa wigi iliyo ndogo na yenye kubana sana, hakikisha unapata muda wa kupata hewa na nywele zako zinapakwa mafuta kuepuka ukavu wa ngozi ya kichwa na nywele kukatika.
Kwa hiyo kama utaamua kuvaa wigi uhakikishe imetengenezwa kwa viwango vya ubora unaotakiwa na inapitisha hewa ya kutosha ya oksijeni.
Endapo mwanamama atachagua kuvaa wigi, asisahau kuwa nywele zake za asili zinahitajika matunzo na zingatie wakati wa kununua aina ya wigi au nywele ya bandia inayomfahaa kwa kununua nywele bora.
Hata hivyo mwananchiscoop ilifanya mahojiano na baadhi ya wadada wanaopenda kuvaa wigi na kusuka nywele bandia wengi wao walisema wanafanya hivyo ili kuongeza mvuto, waonekane nadhifu na maridadi.
Walisema kupitia elimu hii wanayoipata katika jarida hili sasa wametambua juu ya umuhimu wa kununua kitu kilichobora ili wasipate madhara ya kiafya.
Mwishoo…..
Leave a Reply