Madam Lulu, mwalimu mwenye muonekano tofauti

Madam Lulu, mwalimu mwenye muonekano tofauti

Walimu wengi huwa na mitindo ya kufanana kwenye mavazi, mavazi ya heshima yasiyiweza kuonesha maungo yao ni sheria kwao.

Lakini hiyo imekuwa tofauti kwa mwalimu Lulu maarufu kama madam B kutoka Afrika ya Kusini, madam huyu amekuwa na mitindo tofauti ya kimavazi hata akiwa darasani.

Lulu alipata umaarufu baada ya picha zake ku-trend katika mitandao ya kijamii kuhusiana na mavazi yake, ambayo wengi wamedai kuwa  hayafai kwa mwalimu.

Mwanadada huyo inadaiwa kuwa ni mmoja wa walimu matajiri zaidi nchini Afrika Kusini, kutokana na watu wengi kuonekana wakipinga uvaaji wake madam Lulu alivyunja ukimya na kuwajibu wote wanao mpinga.

Katika majibu yake alisema,

“Sifundishi mtoto wako kwa hivyo tafadhali, acha na  unasahau kitu kimoja, sifundishi watoto wa umri wako, wanafunzi wangu hawana akili potovu ulizonazo”

Kufuatia baadhi ya Vyombo vya Habari nchini humo ikiwemo The City Media anaripotiwa kujitengenezea mali nje ya kazi yake ya ualimu na amepata sehemu kubwa ya mapato yake kutokana na kazi yake kama mshawishi wa mitandao ya kijamii na mfanyabiashara wa vipondozi.

Lulu ana Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Elimu na Shahada ya Uzamili ya Hisabati. Mpaka sasa mwanadada huyo haijajulikana amesoma chuo gani lakini inasemekana huenda alisoma katika chuo kikuu jimbo la Kwazulu-Natal ambako alikulia.

Kuhusu mahusino yake, familia na chochote kinacho husiana na yeye cha binafsi ameamua kutoweka mitandaoni, japo hapo awali alitajwa kutoka kimapenzi na marehemu Ginimbi Kadungure.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags