Madaktari waanza mgomo, Nigeria

Madaktari waanza mgomo, Nigeria

Chama cha madaktari kutoka nchini nigeria (nard) imeanza mgomo unaohusisha madaktari wa hospitali za serikali kutokana na mamlaka kutotimiza mahitaji yao ikiwemo maboresho ya mishahara yao.

Aidha upande wa serikali umedai mgomo huo sio halali na watakaoshiriki hawatalipwa kwa kuwa kuna mazungumzo yanaendelea  na madaktari, kauli ambayo imepingwa na Rais wa chama hicho dkt Emeka Orji akidai hakuna kinachoendelea baina ya pande hizo mbili.

Sambamba na hayo madaktari wanataka serikali ifute muswada unaoelekeza wataalamu wa afya wanaohitimu mafunzo vyuoni hawatakiwi kwenda nje ya nchi hadi wawe wamefanya kazi kwa muda wa miaka mitano.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags