Mabaki ya Titan ndogo yapatikana

Mabaki ya Titan ndogo yapatikana

Mabaki ya ‘meli’ ndogo ya Titan Ocean Gate iliyokuwa inafanya safari zake kwenda kutazama ‘meli’ maarufu iliyozama ya Titanic, yameonekana kutoka chini ya bahari baada ya abiria wote kufariki katika ‘meli’ hiyo.

Inadaiwa kuwa mabaki hayo yalipatikana tangu wiki iliyopita lakini imetangazwa siku ya jana Jumanne kuwa Wahandisi wa Usalama Baharini wamepata vipande vya ziada kutoka katika kina cha bahari ya Atlantiki.

Walinzi wa pwani walipata baadhi ya mabaki ambayo bado hayajatambuliwa pia walipata mabaki yanayosemekana kuwa huenda yakawa mabaki ya binadamu ambayo yatafanyiwa uchunguzi zaidi.

Ikumbukwe watu ambao walifariki katika meli hiyo ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Ocean Gate, Stockton Rush, abiria wengine ni pamoja na Paul Henri-Nargeolet, Hamish Hardin, Shahzada Dawood na mwanaye Suleman.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags