Maafisa washtakiwa kwa kukadiria kodi

Maafisa washtakiwa kwa kukadiria kodi

Mahakama ya wilaya ya Kilwa mkoani Lind imewatia hatiani Maafisa Forodha wa TRA, Sultan Ali Nasor na Silver Maximillian kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kutofanya tathmini sahihi ya kodi iliyosababishia mamlaka hasara ya Tsh. Milioni 9.269.

Washtakiwa hao walifanya tathmini ya kodi kwa madumu ya mafuta ya kupikia 200 tu badala ya 500 ya lita 20 kila moja, yaliyoingizwa kutoka Zanzibar ikiwa ni mali ya mfanyabiashara Athumani Ahmadi Simba

Aidha Bw. Simba alishtakiwa kwa kushindwa kulipa kodi ambapo alikiri kosa na kulipa Tsh. 9,269,066.38/-, huku washtakiwa wengine wakihukumiwa miaka tatu jela kwa kosa la kwanza na la pili kila mmoja au kulipa faini ya Tsh. 250,000/= kila mmoja kwa kila kosa, na kifungo cha nje mwaka mmoja.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags