Lungu alaani serikali kuchukua mali zake

Lungu alaani serikali kuchukua mali zake

Rais wa zamani nchini Zambia Edgar Lungu, amelaani hatua ya serikali ya nchi hiyo, kuchukua mali mbalimbali zinazohusishwa na familia yake, na kusema kuwa kitendo hicho kimechochewa kisiasa.

Mali hizo zilichukuliwa kwa mujibu wa sheria ya utaifishaji wa mapato ya uhalifu ya mwaka 2010, ambayo inaruhusu serikali kuchukua mali ambayo inaamini ilipatikana kwa njia zisizo halali.

Wakili wa Lungu, Makebi Zulu anaeleza kuwa yeye mteja wake hajapewa notisi ya mchakato wowote, ulio mbele ya mahakama yoyote kuhusu kukamatwa kwa mali zake.

Akizungumza na vyombo vya sheria tangu uchunguzi huo uanze mwaka jana, Zulu alisema mteja wake ametoa maelezo ya kutosha jinsi alivyopata mali hizo nakuwa serikali inazuia kwa makusudi taarifa hizo ili kuwaaibisha Lungu, mke wake Esther Lungu, na watoto wao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags