Lulu: Jua Kali haina uhusika na maisha yangu

Lulu: Jua Kali haina uhusika na maisha yangu

Mwigizaji wa Bongo Movie Elizabeth Michael ‘Lulu’ wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 22, jijini Dar es Salaam amesema kuwa uhusika anaocheza kwenye tamthilia ya Jua Kali hauna uhusiano wowote na uhalisia wake badala yake anafikisha ujumbe kwa jamii.

“Mimi ni msanii ninapopewa uhusika wowote sihoji kwa sababu hizi tunazozicheza kwenye tamthilia, movie ni vitu ambavyo vipo kwenye jamii ambavyo nyie hamvioni kwa sababu vinafichwa, sisi hizi stori siyo za kusadikika ni vitu vinavyoendelea huku chini sisi tunakuja tuu kuviwasilisha.

"Kwa hiyo mimi sina tabia ya kuchagua uhusika nzuri au mbaya naamini mimi nimepewa neema ya kuwa mtu anayefikisha ujumbe, siyo kila ujumbe utakuwa mzuri mimi ni mjumbe tu ukiwa mbaya nakupa ukiwa mzuri pia nakupa wewe utaamua uufanyaje,” amesema Lulu.

Lulu kwenye tamthilia hiyo anaigiza kama Maria mwanamke ambaye hajatulia na mwanaume mmoja kwenye mahusiano.
Aidha mwigizaji huyo amefunguka kuhusiana na minong’ono inayodai huenda mwigizaji Mimi Mars akarudi kwenye Tamthilia ya Jua kali na kuchukua uhusika wake.

“Kila mtu anajua kuwa hizi ni kazi na kila kazi ina makubaliano mimi sina wasiwasi wowote kwa sababu nayajua makubaliano yangu na yeye kama amepata makubaliano mengine ni neema ni baraka tuendeleze kazi na kazi ziendelee,” amemalizia Lulu

Utakumbuka kuwa awali uhusika anaocheza Lulu kwenye tamthilia ya Jua Kali ulikuwa unachezwa na Mimi Mars kisha baadaye msanii huyo alitoka katika tamthilia hiyo ndipo Lulu akachukua uhusika.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags