Lukamba ampa Cecy talaka tatu

Lukamba ampa Cecy talaka tatu

Alooooweeeh! Alooootenaaah! Bwana bwana naona kama disemba imeanza kibabe ama nini maana sio pouwa huko mjini Instagram kumekuwa kwamoto sana kutokana na mastory makubwa makubwa, basi bwanaa…

Mpiga picha Maarufu na Msanii wa muziki Lukambakama inavyojulikana kuwa ameachia wimbo wake mpya uitwao nitazoea, basi bwana Mbali na hivyo amethibitisha kumpa Talaka 3 aliekuwa Mke wake Cecy.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Lukamba amelithibitisha hilo wakati akiutangaza wimbo wake mpya na kuambatanisha na Talaka hiyo ambayo aliitoa Novemba 11,2022.

Mmmmh! Makubwa haya bwana talaka hiyo ilikuwa imeandikwa hivii “Mimi Ashraf Haji Lukamba leo tarehe 24/11/2022 natoa talaka tatu(3) kwa Cecilia Godfrey Vatinga kuanzia leo sio mke wangu, natoa talaka hii kwa akili zangu timamu bila ya kushurutishwa na mtu yoyote, nakutakia kila la kheri katika maisha yako” ameandika Lukamba






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags