Liverpool yazindua uzi wa mwaka 1984

Liverpool yazindua uzi wa mwaka 1984

Liverpool imezidua jezi mpya kwa ajili ya msimu ujao 2024-25, huku mashabiki wakiifananisha na ya mwaka 1984 kutokana na muundo wake.

Liverpool inajiandaa na maisha  bila kocha wake wa sasa Jurgen Klopp, huku Arne Slot kutoka Feyenoord akitarajiwa kuingia kwenye timu hiyo kwa ajili ya kuendeleza kazi nzuri ya Mjerumani huyo aliyofanya kwa miaka tisa.

Wachezaji mastaa wa timu hiyo, Virgil van Dijk na Mohamed Salah ni kati ya wale walioonekana kwenye picha ya kutambulisha jezi hizo, huku kukiwa na maswali mengi kuhusu mustakabali wao kwa ajili ya msimu ujao kwenye timu hiyo baada ya tetesi kusema kuwa wanatarajia kuondoka.

Hata hivyo, pamoja na mashabiki kwenye mtandao kuamini kuwa ni mtindo wa miaka mingi iliyopita, Liverpool imesema kuwa imeiga baadhi ya vitu kwenye jezi ya timu hiyo ya mwaka 1984 iliyokuwa na mafanikio makubwa.

Mwaka huo Liverpool ilifanikiwa kutwaa makombe makubwa matatu, Ligi Daraja la Kwanza, Kombe la Ligi pamoja na Kombe la Ulaya, ikiwa chini ya kocha Joe Fagan.

Akizungumzia jezi hizo, Van Dijk amesema amefurahi kuona anavaa jezi hiyo, kwa kuwa Liverpool ni timu ya kihistoria.

"Nimefurahishwa sana na jezi hii, mimi ni shabiki mkubwa sana wa aina hii ya jezi, hii ni timu ya kihistoria na ninafurahi kuona tunahimiza hilo," alisema nahodha huyo wa Liverpool.

Wengine ambao wameonekana kwenye picha wakiwa wamevaa jezi hiyo ya nyumbani ni Ibrahima Konate, Darwin Nunez, Alexis Mac Allister na Joe Gomez.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags