Lil Yatchy: Muziki wa Hip-hop una hali mbaya

Lil Yatchy: Muziki wa Hip-hop una hali mbaya

Rapa kutoka nchini #Marekani, #LilYatchy amedai kutoridhishwa na uelekeo wa muziki wa Hip-hop duniani na kusema kuwa muziki huo upo kwenye hali mbaya.

‘Rapa’ huyo ametoa maoni yake kuhusu hali ya muziki huo kwa dunia nzima akidai kuwa muziki huo kwa sasa una hali mbaya na haridhishwi kabisa akisema kuwa muziki huo umekuwa wa kuigana na hakuna ubunifu tena.

Aliendelea kusisitiza kuwa sasa hivi wasanii wamekuwa wakilipua muziki huo na nyimbo zisizo na ubora ndiyo zimekuwa zikipewa kipaumbele.

Ikumbukwe kuwa msanii mwenye umri wa miaka 26 mwezi uliopita alitoa wimbo wake wa ‘The secret recipe’.

 

 Una maoni gani kuhusu kauli hii?
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags