Lil Rod: Diddy na wenzake wananitishia maisha

Lil Rod: Diddy na wenzake wananitishia maisha

Siku moja baada ya habari kuvuja kuhusu Diddy kuwasilisha ombi la kufuta kesi ya unyanyasaji wa kijinsia iliyofunguliwa na mtayarishaji Rodney "Lil Rod" Jones, dhidi yake, mtayarishaji huyo ameibuka tena kwenye mitandao na kudai kuwa Diddy na wenzake wanamtishia maisha.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Rolling Stone’ Lil Rod amefunguka akidai kuwa katika miezi michache amekuwa akijificha, ametengwa lakini pia Diddy na wenzie wanamtishia maisha.

“Hapa nipo, nasimama kwa ajili ya haki, kwa kile ninachoamini kuwa ni sahihi kwa maisha yangu, ninalipizwa kisasi kwa hilo. Nimetengwa, hakika. Nimekuwa na mawazo ya kujitoa uhai kwa siku nyingi, wiki, na miezi. Ni muziki ndiyo umeniweka hai maisha yangu yote.

"Sijawahi kupokea mashambulizi mengi kwa wakati mmoja kama hivi sasa. Diddy ana watu wengi kwenye malipo yake katika nafasi nyingi tofauti na ndiyo anawatumia kunitishia” amesema Lil Rod

Ikumbukwe kuwa Lil Rod alijitokeza kwa mara ya kwanza Februari mwaka huu akimshutumu Diddy kwa kujihusisha na madai ya unyanyasaji wa kijinsia pamoja na kujihusisha kwenye biashara na matumizi ya dawa za kulevya, lakini Combs amekanusha vikali madai hayo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags