Lijue tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Lijue tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya mapenzi kikamililifu au kushindwa kusimamisha vizuri. Shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili, homoni, neva, misuli, hisia na mirija ya damu.

Tatizo hili huripotiwa kuwa katika wanaume watano (5) basi mmoja kati yao ana tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ambapo ni sawa na asilimia ishirini (20%).

Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kutokuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalohitaji tiba.

Tatizo hili ni kubwa, ambapo watafiti wanaripoti ya  kwamba wanaume wengi wenye umri kati ya miaka 35 na kuendelea ndio wanaosumbuliwa kwa kiasi kikubwa,

Tatizo hili lina athari nyingi sana zikiwemo za kisaikolojia na kifamilia pia, ikiwemo kupelekea mahusiano kutokuwa imara na mara nyingine kuvunjika kabisa.Hata hivyo tatizo hili linatibika na kupona kabisa kwa aliyeathirika.

CHANZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata tatizo la nguvu za kiume nayo ni pamoja na;

  • Kuwa na halemu (Cholesterol) na shinikizo la damu (B.P) au ugonjwa wa moyo.
  • Kuvuta sigara na unywaji wa pombe uliokithiri.
  • Uzito kupita kiasi na unene uliozidi.
  • Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi.
  • Kuwa na msongo wa mawazo na wasiwasi.
  • Matumizi ya madawa mbalimbali ya hospitali mfano dawa za kutibu msongo wa mawazo.
  • Umri hasa wazee.
  • Kuwa na tatizo la kibofu.
  • Tabia za kujichua kwa muda mrefu.(punyeto)
  • Kutopata usingizi mzuri.
  • Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibia magonjwa kama kansa, vidonda vya tumbo, moyo, kisukari, B.P, na magonjwa mengine.

DALILI ZA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

  • Kushindwa kusimamisha uume vizuri.

Kushindwa kabisa au kupatikana udhaifu katika kusimamisha uume ni moja ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume hii inaweza kusababishwa na maradhi yanayohusiana na mzunguko wa damu, sababu za kisaikolojia kama vile mawazo n.k

  • Kutokuwa na hamu na tendo la ndoa.

Kushindwa kurudia tendo la ndoa ikiambatana na kuwahi kufika kileleni haraka

  • Kupata udhaifu na uchovu wa mwili wakati wa tendo la ndoa

JINSI YA KUEPUKANA NA KUPATA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

  • Fanya mazoezi – Angalau dakika 30 kwa siku
  • Kula vyakula asilia na usile vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
  • Tibu magonjwa yako yanayokuweka hatarini kama kisukari, moyo, punguza unene na mengine
  • Punguza kiwango cha halemu (choresterol) au mafuta yaliyozidi
  • Usivute sigara
  • Punguza matumizi ya pombe
  • Punguza mawazo
  • Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali
  • Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9
  • Usitumie dawa zenye kemikali nyingi huathiri mfumo wa uzazi
  • Kunywa maji ya kutosha

VYAKULA VINAVYOONGEZA NGUVU ZA KIUME KWA HARAK

Vyakula tunavyokula vina mchango mkubwa katika kuimarisha nguvu za kiume, hivi ni baadhi ya vyakula vilivyothibitika kuwa na matokeo mazuri sana na ya haraka katika kuimarisha nguvu za kiume:

1.Ndizi Mbivu

Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamini B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Kwa matokeo mazuri , kula ndizi 2 hadi 3 zilizoiva kila siku.

  1. Tikiti Maji

Ulaji wa Tunda hili pamoja na kutafuna kokwa zake mara kwa mara una matokeo mazuri katika kuimarisha nguvu za kiume.

  1. Kitunguu Swaumu

Kitunguu swaumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi.

 

 Imeandaliwa na Mark Lewis






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags