Lewis Hamilton avunja rekodi

Lewis Hamilton avunja rekodi

Dereva wa timu ya magari ya Mercedes Muingereza Lewis Hamilton ameshinda mbio za Langalanga (Formula 1) nchini Urusi (Russian Grand Prix) na kuweka rekodi ya kuwa dereva wa kwanza kushinda mbio mara 100.

Mbio hizo zilizomalizika jioni ya jana Septemba 26, 2021 huko Sochi, zinamfanya Lewis aongoze msimamo wa madereva akiwa na pointi 246.5

Hamilton sasa ameshinda tuzo yake kubwa ya mia moja (100) katika mbio za langa langa baada ya kumshinda mpinzani wake Birt Lando Norris ikiwa imebakia mizungo miwili tu kumaliza mbio hizo.

Hapo awali ilionekana kuwa Norris ataweza kuwa dereva kijana zaidi wa kiingereza kuwahi kushinda mbio za Formula 1 hadi mvua ilipo onyesha na Norris akaamua kua anabadili sana matairi ili abaki kua na matairi makavu akihofia kuteleza, hali iliyozidi kumuweka kwenye nafasi ngumu na kujikuta akimwacha Hamilton apite na kuchuchua uongozi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags