Lebron akataa mwanaye kumuita baba wakiwa uwanjani

Lebron akataa mwanaye kumuita baba wakiwa uwanjani

Baada ya LeBron na mwanaye Bronny James kusainiwa katika timu moja ya mpira wa kikapu ya Lakers nchini Marekani, LeBron ametoa ufafanuzi jinsi mwanaye atakavyomuita wakiwa kwenye mazingira ya kazi.

Kwa mujibu wa Tmz LeBron aliulizwa swali kuhusiana na mwanaye kumuita baba watakapokuwa uwanjani pamoja ndipo akajibu kuwa hatoruhusu kuitwa baba kwenye eneo la kazi.


"Hapana, hawezi kuniita baba kazini. Mara tu tunapotoka nje ya eneo la uwanja milango ikafungwa basi hapo naweza kuwa baba tena, tukiendesha gari pamoja nyumbani anaweza kuniita baba lakini hapa anaweza kuniita ‘2-3’ au Bron,” amesema LeBron mwenye umri wa miaka 39.

Aidha alitania kwa kudai kuwa kijana wake huyo mwenye umri wa miaka 19 anaweza tu kumuita ‘G.O.A.T’ endapo atapenda.

Utakumbuka kuwa mapema mwezi Juni kijana wa LeBron James, Bronny James alisajiliwa kwenye timu anayochezea baba yake






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags