Lebron afikiria kustaafu kucheza mpira kikapu

Lebron afikiria kustaafu kucheza mpira kikapu

Nyota wa mpira wa kikapu kutoka nchini Marekani anayekipiga NBA, LeBron James (39) ameweka wazi kuwa anampango wa kupumzika kucheza mchezo huo.

LeBron ameyasema hayo wakati akiwa kwenye mahojiano ya hivi karibuni ambapo alieleza kuwa muda si mrefu hatocheza tena kwani miaka 21 dimbani inamtosha, japo hajui ni lini atatangaza kustaafu kwake rasmi, lakini amedai kuwa atafanya hivyo muda si mrefu.

LeBron alianza rasmi kucheza mpira kikapu mwaka 2003 ambapo alikuwa akikipiga katika ‘timu’ ya ‘Cleveland Cavaliers’ na sasa anachezea ‘timu’ ya ‘Los Angeles Lakers’ aliyosaini nayo mkataba toka mwaka 2018.

Hata hivyo ndani ya miaka 21 mchezaji huyo amewahi kuondoka na Tuzo kadhaa kutokana na makubwa aliyoyafanya katika mchezo huyo zikiwemo ‘NBA All-Star Game Kobe Bryant MVP Award’, ‘Best Record-Breaking Performance ESPY’, ‘USA Basketball Male Athlete of the Year’, ‘Mr. Basketball USA’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags