Lady Jaydee kutoa msaada wa masomo kwa watu watano

Lady Jaydee kutoa msaada wa masomo kwa watu watano

Msanii wa Bongo Fleva Lady Jaydee ametoa nafasi tano za ufadhili wa masomo kwa ngazi ya chuo kwa watu ambao wazazi au walezi wao hawana uwezo wa kumudu gharama za kulipia ada.

Mwanamuziki huyo ametangaza fursa hiyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijami kuwa anahitaji watu watano ili kuwanufaisha kimasomo kupitia taasisi yake ya Lady Jaydee Foundation.

Msanii huyo ameandika katika ukurasa wake wa Instagram "Nafasi za masomo kwa wanafunzi watano wa chuo. Haijalishi jinsia, ila kwa kipaumbele watachukuliwa wasichana 3 na wavulana 2."
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags