Lady jaydee, afunguka maandalizi ya ‘mambo matano’, siri ya kudumu kwenye game na utunzi wake

Lady jaydee, afunguka maandalizi ya ‘mambo matano’, siri ya kudumu kwenye game na utunzi wake

Hellow watu wangu wa nguvu tumekutana tena hapa kwenye segment yetu pendwa ya Burudani wazee wa kuburudika hili ndilo chimbo letu la kipekee.

Kama kawaida wanangu huwa hatuachi kitu kikalala tunaogopa kitachacha ndiyo ikivyo kwenye wimbo wa mkali dada mkuu, Lady Jaydee, mwenyewe amekuwa na majina mengi kutokana na ukali wa ngoma zake na ukongwe kwenye game.

Mwananchi Scoop tukamvutaa kwa ajili ya kufahamu mengi hasa kuhusiana na kazi yake mpya aliyoiachia “Mambo matano”.

Maswali ya kichokozi kama unavyofahamu hatukuacha kumuuliza dada mkuu kwanza kabisa tulitaka kufahamu kuhusiana na aina ya wimbo aliyoutoa kuwa tofauti na nyimbo nyingi zinazotoka sasa kwani wengi wamejikita kwenye Amapiano.

Bila kupepesa macho Lady Jaydee alijibu kwa kusema , “sijawahi kufuata trend, huwa na set trend yangu mwenyewe ili watu wengine ndiyo waifuate. na ndiyo maana halisi ya kuitwa dada mkuu”.

Lakini hatukuishia hapo msomaji wetu, Jide alifichua na kutupa siri ya kile kilichokuwa kikifanyika wakati wa kuandaa wimbo wa ‘Mambo Matano’ na kudai kwa ujumla umetengenezwa na watu watatu.

Huku yeye akiwa jikoni wakati huo na kisha baadaye wimbo ulivyo kamilika aliweza kupita na mistari kama iliyo bila shida yoyote na baada ya kukamilia wimbo ukasikilizwa na kwa takribani miezi mitatu kabla ya kutoka.

Kama ilivyo kawaida Jide hakuacha kutoa somo na kudai kuwa msanii unatakiwa kuwa na nembo yako ambayo inakutambulisha ambayo itafanya watu waelewe kazi unayofanya na ndiyo maana ‘Mambo Matano’ ilivyotoka wengi walisema huyo ndiyo Jide waliyemzoea.

Dada mkuu akaendelea kutusanua ambavyo tulikuwa hatuvijui kumuhusu yeye, na kudai kuwa kipindi cha nyuma alikuwa akipata shinda kwani watu walikuwa wakiweka mitazamo yao kwenye tunzi za nyimbo zake, akasema,

“mwanzo ilikuwa inanisumbua sana ukitoa wimbo watu wanasema umemuimba mtu fulani, inahusiana na hivi, au ni maisha yangu, tutoe dhana ya kuwa wimbo unaotoka ni kwa ajili ya kumlenga mtu.”

Wale wa kuweka mawazo yao kwa kuwa na dhana za kutafsiri nyimbo la kwenu hilo, aliendelea kutupa siri inayofanya awepo kwenye game muda wote, amesema kuwa  maisha hayatofautiani sana kwa hiyo anatoa nyimbo zinazolenga maisha ya kweli ya kila siku, na na kugusa mioyo ya watu.

Na mara chache sana huimba nyimbo zisizokuwa na  maana yoyote kwani yeye ni msanii ambaye mtu akisikia wimbo wake basi lazima atapata ujumbe .

Tulimaliza kwa kutaka kufahamu kuhusiana na kilicho msukuma hadi kutoa msaada kwa watoto kusoma vyuo vikuu akasema, “sababu ni kuwasaidia watoto wenye akili wasio na uwezo wa kusomeshwa au kujisomesha.”

 

Mimi sina cha kuongezea kwenye hilo zaidi niseme tu ‘Mambo Matano ‘ ni wimbo mkali sana na kama ambavyo amesema Jide kuwa unapatikana kwenye Platform mbalimbali, cha kufanya tafuta muda wako uutafute kisha sikiliza naimani utanishukuru baadaye. Tchaoo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post