Kuwa Jide au Mona ni ushujaa

Kuwa Jide au Mona ni ushujaa

Huenda Mungu akawa na wapinzani wengi zaidi, maana kujichubua ni kupinga uumbaji wake, kwamba wameumbwa visivyo! Hii leo siyo wadada tu wanaojichubua. Also men do it, sijui ndiyo kuwaiga wenzetu wa kule Congo? Inakera, wengine vidole kama mahindi ya kuchoma.

Wazungu wameshajua udhaifu wetu watu weusi. Kwenye mitandao ya kijamii kuna utundu wameweka wa kusafisha picha ya mtu mweusi kuonekana mweupe, au mwenye ngozi nyororo lakini hakuna utundu wa kumfanya mweupe awe mweusi.

Hivi juzi kuna mchezo flani uliitwa “Ten Years Challenge”, yaani mtu anaweka picha yake ya miaka 10 nyuma na ya sasa. Kisha anasindikiza na maneno ya #TenYears Challenge. wanawake wengi wa mjini waliupuuza maana haukuwa rafiki na ngozi zao za kale.

Kwa mfano Instagram unaweza kudhani kila msichana ni mweupe na hana chunusi. Wanafurahia kujidanganya, ni kama kulewa ili upunguze mawazo wakati mawazo hayaishi. Msichana wa kizazi hiki kuwa Monalisa au LadyJaydee, yaani ngozi kubaki vilevile ni ushujaa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags