Kutana na Lammer mlemavu aliyekataa kustaafu kazi

Kutana na Lammer mlemavu aliyekataa kustaafu kazi

Chef Peter Lammer ni mpishi maarufu kutoka nchini Ujerumani ambaye alipata ajali ya pikipiki mwaka 2010 akiwa na umri wa miaka 44 ambapo baada ya kupatiwa matibabu ya muda mrefu Daktari wake alimtaka astaafu kazi hiyo ya upishi kufuatiwa na kutoweza kutembea, lakini kwa kuwa Lammer yeye anapenda kupika aliamua kuvumbua kiti ambacho kingeweza kumsaidia aendelea na kazi yake.

Kupitia mahojiano yake Lammer ameeleza kuwa yeye hupendelea kuendesha pikipiki na kupika hivyo basi ingemuwia vigumu kuacha kuingia jikoni kabisa, ambapo aliweka wazi kuwa amevumbua kiti hicho kwa ajili yake na wapishi wengine ambao wamepitia kwenye changamoto hiyo aliyoipitia.

Peter Lammer amevumbua kifaa hicho ambacho kinajulikana kwa jina la ‘Standing Ovation’ ambacho kinaweza kumzungusha mpishi asiyeweza kutembea katika kona zote za jiko.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags