Kuona pambano la Tyson na Jake sh 5 bilioni vip

Kuona pambano la Tyson na Jake sh 5 bilioni vip

Mabondia wa ngumi za kulipwa kutoka Marekani Mike Tyson na Jake Paul wanaotarajia kuzichapa Julai mwaka huu siku ya jana wametoa bei ya tiketi za VIP ambapo ‘tiketi’ moja inagharimu kiasi cha dola 2 milioni ikiwa ni zaidi ya Sh 5 bilioni.

Ukinunua ‘tiketi’ hiyo utafanikiwa kupata huduma za kipekee ambazo ni kupiga picha na mabondia hao kabla ya pambano kuanza, kupewa glavu zilizosainiwa na mabondia, chumba cha faragha chenye huduma ya hali ya juu, pia utapata fursa ya kupanda jukwaani wakati wa upimaji uzito wa mabondia.

Pambano la Tyson (58) na Jake (27) linatarajiwa kufanyika Julai 20 katika uwanja wa AT&T uliopo jijini Texas nchini Marekani pia litaoneshwa live kupitia mtandao wa Netflix.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags