Kunywa bia kunasaidia kujilinda na magonjwa ya moyo

Kunywa bia kunasaidia kujilinda na magonjwa ya moyo

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imeshauri jamii kupenda kufanya mazoezi, kupunguza kula vyakula vya sukari, wanga na kusisitiza kwa wanywaji wa bia, kunywa angalau tatu kwa siku ili kujilinda na ugonjwa wa moyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge amesema hayo leo Jumatatu Julai 10, 2023 katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba). Amesema kuna ongezeko la wagonjwa wa moyo nchini.

“Asilimia kubwa ya wanaolazwa hospitali ni wagonjwa wa moyo na shinikizo la damu,” amesema

Dk Kisenge ameshauri jamii kuzingatia kula lishe bora hasa mboga za majani na matunda, kupunguza vyakula vya wanga na sukari. “Unywaji bia, angalau mnywaji anywe bia tatu kwa siku,” amesema.

Mkurugenzi huyo amesema Watanzania wawe na kawaida ya kucheki afya zao mapema hii inasaidia kujijua na kupunguza madhara. Kwenye banda letu tunatoa huduma hizo na elimu ya afya ya moyo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags