Kumbe Messi hajamsaliti mkewe

Kumbe Messi hajamsaliti mkewe

Familia na watu wakaribu wa mchezaji wa ‘klabu’ ya #InterMiami #LionelMessi, wamekanusha vikali taarifa inayodaiwa kuwa mchezaji huyo amemsaliti mke wake #AntonelaRoccuzzo.

Kwa mujibu Gazeti la Brazil Direto Do Miolo inaelezwa kuwa kumekuwa na taarifa kuwa uhusiano huo uliodumu kwa miaka 15 unakabiliwa na mgogoro kutokana kuwepo kwa tetesi kuwa nyota huyo wa Inter Miami alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwandishi wa habari kutoka Argentina, #SofiaMartinez.

Lakini taarifa hizo zimepingwa vikali na familia ya mchezaji huyo na kudai kuwa uvumi huo siyo wa kweli na wamechukizwa na kitendo hicho kinachoendelea katika vyombo vya habari mbalimbali.

Messi na Roccuzzo wamefahamiana tangu wakiwa na umri wa miaka mitano na walifunga ndoa mwaka 2017 na kubahatika kupata watoto watatu Thiago, Mateo na Ciro.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags