Kukonda kwa Bautista kwageuka gumzo

Kukonda kwa Bautista kwageuka gumzo

Mwonekano mpya wa mwigizaji na nyota wa WWE, Dave Bautista umewapa wasiwasi mashabiki, baada ya picha yake kusambaa mitandaoni ikumuonesha amepungua (amekuwa mwembamba) kuliko watu walivyomzoea.

Picha ya mwigizaji huyo mwenye umri wa miaka 55 imemuonesha akiwa mwembamba zaidi kuliko kawaida huku baadhi ya mashabiki wakihisi huenda picha hizo zimeeditiwa.

Hata hivyo akiwa kwenye mahojiano na ‘Universe’ mwigizaji huyo hakutaka kufunguka zaidi na kudai kuwa uzito aliokuwa nao sasa ni mdogo zaidi ya ule aliyokuwa nao wakati ana miaka 19.

Kwa mujibu wa baadhi ya tovuti mbalimbali zimebaini kuwa picha hiyo ya Bautista ilipigwa katika tamasha la Kimataifa la Filamu la Toronto ‘The Last Showgirl’ lililofanyika siku mbili zilizopita.

Bautista alianza kujizolea umaarufu kupitia mieleka mwaka 2002 hadi 2019, na kuamua kujikita katika uigizaji rasmi ambapo ameonekana katika filamu kama ‘My Spy’, ‘The Killer's Game’, ‘Knock at the Cabin’, ‘Escape Plan’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags