Kukabiliana na tatizo la ajira kwa wahitimu wa vyuo

Kukabiliana na tatizo la ajira kwa wahitimu wa vyuo

Na Michael Onesha

Mwandishi wa vitabu Joel Nananuka katika kitabu chake cha Ishi ndoto yako ‘Ebook’ Aliwahi kusema ndani yako kuna uwezo na hazina kubwa sana ambayo ukianza kuitumia kwa kiwango cha juu itakusaidia sana kutoka hapo ulipo na kwenda kiwango cha juu  cha maisha yako.

Hivyo hivyo kwa wewe mwanafunzi wa chuo unatakiwa kufanya kazi kwa bidii tenga muda mzuri wa kufanya mambo yako, chuo kikuu ni ngazi ya juu zaidi ya elimu nchini Tanzania na duniani kwa ujumla ambayo inamuwezesha mwanafunzi (Mwanachuo) kupata maarifa na ujuzi maalumu.

Kwa miaka ya hivi sasa kumekuwa na tatizo la ajira kwa wahitimu wengi wa vyuo vikuu (Wahitimu wa kuanzia 2015-2023 kwa kiasi kikubwa) ambapo wengi wao wamejikuta wakikaa mtaani bila ya kuwa na kazi za kuwaingizia kipato, jambo linalosababisha wahitimu hao wa vyuo kuilaumu serikali na kuiiona elimu waliopata si chochote kwao na walipoteza muda wao kuitafuta elimu hiyo.

Ni kweli kwamba kwa kawaida serikali inapaswa kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo, lakini ni ukweli uliodhahiri kwamba kuajili wahitimu wote ni ngumu kwa sababu idadi ya wanaohitimu ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa uchumi wa nchi yetu katika ulipaji wa mishahara ni mdogo hivyo serikali haiwezi kuajili wahitimu wote bali inaajili kulingana na ukubwa wa mfuko wake (uchumi).

Kutokana na ukweli kwamba kila mtu angependa awe na ajira baada ya kuhitimu chuo kikuu ni vema kila mwanafunzi wa chuo kuangalia namna ya kupata ajira kupitia elimu aliyonayo kwa mikakati mbali mbali.

Mikakati itakayokusaidia kupata ajira au kujiajiri  baada ya kuhitimu

 

  1. Kuhusisha elimu uliyopata chuoni na mazingira halisia ya jamii.

Hii ina maana ya kwamba kutafuta mahali panapohitaji maarifa aliyonayo muhitimu katika jamii na kuyatumia maarifa hayo kama fursa ya ajira.

Mfano umesomea Uandishi wa habari na kama tunavyojua katika course hiyo kuna vipengele vingi, unaweza kutumia kimoja kukutoa kimaisha, labda ukawa mpiga picha mtaani kwako ukafungua kastudio kadogo ka kuanzia i hope utatoboa tuu, Waswahili wanasema ndondondo si chururu.

  1. Kutofautisha kati ya siasa na elimu.

Suala la wanachuo kuchanganya siasa na elimu zao zinawafanya waamini kuwa serikali ndiyo inasababisha kwa 100% kukosa ajira na ilihali wanapaswa kutumia elimu zao kutengeneza ajira, hivyo basi ukiwa kama mwanachuo ondoa fikra za kuwa serikali ndiyo inayokukwamisha, hii itakusaidia kujitambua na kujiongoza.

  1. Kusomea kozi unazoziweza kwa ufanisi na siyo kusoma kwa mkumbo.

Hii iko hivi wahitimu wengi wa elimu ya vyuo wanashindwa kubuni fursa za ajira kwa sababu maarifa waliyoyapata vyuoni hawana uwezo nayo bali wanauelewa tu hivyo wanapojaribu kubuni fursa wanafanya ovyo kabisa.

Cha kuzingatia kabla hujachagua kozi yoyote jaribu kujipa muda wa kutafakari acha kuishi kwa mikumbo kuwa rafiki yako kaenda kusomea hichi na wewe ufuate, hapana kaa chini jitafakari unataka nini kwenye maisha yako, na ndiyo maana nchi za wenzetu mtoto anaanza kuangaliwa toka yuko mdogo nini anapenda kukifanya basi atakazaniwa humo mpaka atoboe.

  1. Kutumia pesa ya kujikimu ( BOOM) kujenga msingi bora wa maisha baada ya kuhitimu chuo.

Wanachuo wengi wanatumia boom kuishi kwa starehe bila kukumbuka kwamba kuna maisha baada ya chuo hivyo wanapaswa kujenga msingi bora wa maisha yao ya baadaye kwa kuanza kuwekeza katika fursa mbalimbali kama vile:

      Kilimo

      Ufugaji (kuku,bata, mbuzi ) ujasiriamali.

  1. Tumia kipaji ulichonacho kujipatia ajira.

Ni kweli kwamba kila binadamu kabalikiwa kipaji tofauti na mwingine lakini ugumu uko tu kwenye mtu kujua kipaji chake. Kwa wahitimu wa vyuo pia wanaweza kutumia vipaji vyao kujikwamua kiuchumi kwa kuvifanya vipaji hivyo kuwa ajira, mfano;  kuimba, kucheza mziki au mpira, kuchora, kuhamasisha .

MWISHO KABISA

Mwisho japo kwa uchache nipende kutumia nafasi hii kuwakumbusha wanachuo na wahitimu wa vyuo kuwa  wasichague kazi kwa kuziona baadhi siyo za hadhi yao bali wazifanye kuwa za hadhi yao kwa kuzifanya kwa ufanisi na weledi wa elimu zao.

Je wewe umekata tamaa ya maisha kwa kukosa ajira? Ulitamani kusoma lakini ukashindwa kwa kukosa ada? Umesoma lakini umekosa ajira? Miaka inapita na unaona wenzio wanaajiriwa wewe uko tu nyumbani? Je Umejaribu biashara lakini kila wakati unapata tu hasara? Unahisi kukata tamaa? Unahisi Mungu amekuacha? Hapana, usikate tamaa, Mungu hajakuacha.

Jipange tena na uanze upya. Haujakawia bado, kitu kikubwa ni "mtazamo wako" (attitude). Haijalishi mambo ni magumu kiasi gani. Una kila kitu cha kukufanya ufanikiwe, amua kubadili mtazamo wako leo ili ubadili historia ya maisha yako kwani inawezekana, anza sasa.

Wazo lolote ulilonalo, ndoto yoyote uliyonayo unaweza kuanza kuiishi kwa mafanikio kama utaamua kuwa inawezekana. Usikubali hali uliyoipitia huko nyuma iwe kizuizi cha mafanikio yako ya kesho.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post