Kufa kufaana, 50 Cent kuibeba mikoba ya Diddy

Kufa kufaana, 50 Cent kuibeba mikoba ya Diddy

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani 50 Cent anatarajia kurithi mikoba ya Diddy baada ya kampuni ya vinywaji ya ‘Vodka Ciroc’ kumfuta ubarozi Combs.

Kwa mujibu wa ‘Takeout Media’ imeeleza kuwa kampuni hiyo iko kwenye mchakato wa kuisaka saini ya 50 ili kuwa kiongozi wa chapa hiyo ambapo atalipwa dola 100 milioni ikiwa ni sawa na Sh 257.5 bilioni.

Endapo dili hilo litakamilika basi itakuwa ni kampuni ya pili ya vinywaji kwa 50 kuwa barozi ambapo kwa sasa ni barozi wa kampuni ya vinywaji viitwavyo ‘Branson Cognac’.

Ikumbukwe kuwa mwezi Januari mwaka huu Kampuni hiyo ilithibitisha kuwa haitafanya kazi tena na Diddy, ikidai kuwa msanii huyo wa hip-hop alishindwa kutimiza majukumu yake ya kimkataba.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post