Kuchukia kufua kulivyomfanya Channing avae nguo mpya kila siku

Kuchukia kufua kulivyomfanya Channing avae nguo mpya kila siku

Mwigizaji kutoka Marekani Channing Tatum amefunguka kuwa aliwahi kununua mashati kwa mwaka mzima kutokana na kuchukia kufua.

Channing Tatum ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye moja ya mahojiano yake hivi karibuni akiweka wazi kuwa anachukia sana kufua nguo kiasi kwamba aliamua kununua shati mpya kila mara kwa mwaka mzima ili kuepukana na kazi hiyo.

“Nilikuwa na mwaka mmoja niliouita 'mwaka wa fulana nyeupe mpya.'Sidhani kama niliwahi kufua nguo hata mara moja kwa mwaka huo. Niliamua tu kuvaa fulana nyeupe ambazo nilikuwa nimenunua, nilikuwa nikijisemea tu nitavaa hii mara mbili kwa wiki.

"Mwaka wa fulana nyeupe mpya ulikuwa ni mwaka 1999 au 2000 ulikuwa mzuri sana kwa kweli” alisema mwigizaji huyo mwenye umri wa miaka 44.

Aidha aliongezea kwa kudai kuwa hadi sasa ni baba wa mtoto mmoja lakini bado anapendelea kuvaa shati nyeupe za kawaida na zilizochakaa kiasi kwa sababu zinamfanya ajione wa kawaida huku akitania kuhusu suruali zake akidai kuwa anapendelea kuvaa za aina ya Dickies ambazo amekuwa akizivaa tangu akiwa na miaka 18 kutokana na kufiti vizuri makalio yake.

Channing Tatum anatambulika zaidi kupitia filamu alizozicheza ikiwemo ‘White House Down’, ‘G.I. Joe: Retaliation’, ‘Fly Me to the Moon’, ‘Bullet Train’ na nyinginezo kibao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags