Kourtney Kardashian afanyiwa upasuaji wa haraka

Kourtney Kardashian afanyiwa upasuaji wa haraka

Mwanamitindo kutoka nchini Marekani Kourtney Kardashian ameweka wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa alifanyiwa upasuaji wa haraka kwa ajili ya kuokoa maisha ya mtoto wake aliyetumboni.

Kupitia ujumbe huo alitoa shukurani kwa madaktari kwa juhudi walizozifanya za kumuokoa mtoto wake wa kiume, huku akimshukuru mumewe Travis Barker's kwa kusitisha ziara yake.

Upasuaji huo wa (Fetal surgery) ulikuwa ni kwa ajili ya kusaidia na kuboresha matokeo ya muda mrefu ya watoto walio na kasoro maalum za kuzaliwa.

Kwa sababu kasoro hizo mara nyingi huzidi kukua kulingana  ujauzito unavyokua, upasuaji wa fetasi unaofanywa na timu ya wataalamu hulenga kutibu na kuboresha hali ya mtoto akiwa tumboni kabla ya kuzaliwa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags