Konkara: Matamanio yangu kuwa Mchekeshaji mkubwa Afrika

Konkara: Matamanio yangu kuwa Mchekeshaji mkubwa Afrika

 

Jina: Noah Joseph (Konkara)

Birthday: 10TH April

Kazi: Comedian

Konkara, kijana anayefanya kazi ya ucheshi ambaye ameenza rasmi mnamo mwaka 2019 chini ya mwamvuli wa Punch Line Afrika, chini ya Evans Bukuku pamoja na Ahmed Ally, ndiyo waliompokea kijana huyo hadi kufika hatua ya sisi kumtambua.

Majina yake kamili kabisa anaitwa Noah Joseph, maarufu “Konkara” bila shaka clip ambayo ilimpeleka mjini kijana huyu kama utakua unaikumbuka ile clip yake ya wachungaji ambayo alifanya kupitia Cheka Tu, ndiyo iliyoibua zaidi kipaji chake.

Hata hivyo Konkara yuko kwenye maandalizi ya kufanya project yake mpya hivi karibuni inayohusu masuala ya uchekeshaji.                

Ebwana kama unavyofahamu, hakuna kazi ambayo haikosi milima na mabonde kwa upande wake Konkara anasema kuwa anapitia wakati mgumu kwenye kazi yake pindi akiwa anafanya wajibu wake.

“Changamoto kubwa ambayo naipitia kwenye kazi yangu ni pale ambapo unachekesha watu kisha na wao wanakua wanaongea au unaenda kuchekesha sehemu ambayo watu wameshalewa hiyo ni changamoto kubwa kwangu,” alisema.

Licha ya hayo yote, kijana huyo bado hajawahi kupokea tuzo yoyote  kupitia kazi zake ambazo anazifanya, huku matamanio yake ni kuja kuwa mchekeshaji mkubwa barani Afrika.

Sambamba na hayo, Konkara amezaliwa Mbeya, kwenye familia yao yeye ni mtoto wa mwisho kati ya watoto 5, alifanikiwa kupata elimu yake ya msingi katika shule Mabonde na sekondari akasoma Kalobe kisha akajiunga Mbeya university of science and technology (MUST), course ya BA.

Kama unavyojua bwana kila binadamu kwenye haya maisha ana mambo ambayo yanampendeza kwenye nafsi yake na yale mengine ambayo hakubaliani nayo.

Kwa upande wa Konkara bwana, yeye afunguka kupitia Mwananchi Scoop na kudai kuwa jambo ambalo halipendi hili hapa:

“Mimi binafsi huwa sipendi kelele, zinanichukiza sana sana, lakini napenda sana kutembelea maeneo ya fukwe za bahari.”

Ebwana usichokijua kuhusu Konkara ni kwamba yeye ni kijana mpole mnoo, lakini kuhusu masuala ya mahusiano hahaha yeye anasema bado yupo yupo sanaaa, akimaanisha yuko single.

Ebwanaaa eeeh bila shaka utakua umepata udambuu dambu na mambo mbalimbali hasa ya kiburudani ambayo yanamuhusu zaidi kijana huyu, endelea kufuatilia jarida letu kila wiki ili uweze kuwajua mastaa chipukizi mbalimbali.

Kama nawe una kipaji na unataka kuzungumza mawili matatu kupitia magazine bora kabisa ya vijana, tutafute kupitia www.mwananchiscoop.co.tz au tembelea email yangu saphinia96@gmail.com ,ahsantee.

 

 

 

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags