Konde faida zaidi ya hasara

Konde faida zaidi ya hasara

Konde Boy anaonekana ana ‘bato’ na Diamond inamsaidia Konde Boy kuliko Diamondi. Kumbuka DMX na Jah Rule ‘bato’ lao lilimsaidia zaidi Jah Rule na kumtuliza DMX. ‘Bato’ la 50 Cent na Rick Ross pamoja na Kanye West. Wote walimtuliza 50 Cent. Naamini Diamond hakutaka limtokee hilo.

Kitu chochote kikiwa na upinzani watu huegemea upande mmoja. Mara nyingi huegemea upande ambao unaakisi unyonge. Kila ngoma ya Konde Boy, hubebwa na mashabiki wa Diamond. Wale wa kutaka kujua ana jipya lipi Konde?

‘Ene wei’ hizi ‘kiki’ zinaharibu sanaa. Zimevuka mipaka mpaka kuumizana nafsi, waache hizi pigo za ‘kiki’ zaidi kutupa muziki mzuri. Acha muziki mzuri utengeneze ‘kiki’ na siyo ‘kiki’ zitengeneza muziki.

Mtaani kuna bato la 'I Made It' ya Konde Boy na Mapozi Remix ya Mr. Blue. Lakini Blue hana shida na Konde, tatizo kwenye ngoma kuna Diamond.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags